Wakati uandaaji wa onyesho la muziki la Coca-Cola Coke Studio msimu wa tano unaendelea jijini Nairobi nchini Kenya linalojumisha kolabo za wanamuziki wa kitanzania kwa kushirikiana na wanamuziki wa nje, washabiki wa muziki nchini wamezisubiri kwa shauku kolabo hizo.
Burudani za onyesho hili ambalo limepata umaarufu mkubwa nchini kutokana na kufuatiliwa na wapenzi wengi wa muziki kupitia luninga litaanza kurushwa mapema mwezi Septemba.
Kwa upande wa Tanzania wasanii ambao wako ndani ya nyumba ni Rayvanny, Izzo Bizness na Nandy.
Katika onyesho la Coke Studio msimu mwa mwaka jana wakali wa muziki nchini ambao walishiriki walikuwa ni Ally Kiba,Vanessa Mdee,Ben Pol na Fid Q ambao walishirikiana na wanamuziki Wangechi, Maurice Kirya, Victoria Kimani na 2Face.
Msanii Rayvanny (katikati) akiwa na wasanii wenzake wakifanya moja ya Mashup hivi karibuni
Mwanamuziki Izzo Business akiwa amepozi ndani ya studio jijini Nairobi

Baadhi ya wasanii nguli waliopo kwenye matayarisho ya Coke Studio msimu wa tano wakiwa katika picha ya pamoja jijini Nairobi hivi karibuni.
Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...