NA RAYMOND URIO.

Mbunge wa Jimbo la Manonga kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Seif Khamis Gulamali  jana ametembelea kiwanda cha Manonga Ginery kinachohusika na kutengeneza pamba, kilichokuwa kimesimama kwa takribani miaka ishirini (20) bila ya kufanya.

Mapema leo hii Mbunge Gulamali aliwasili katika eneo la kiwanda hicho, iliyopo Jimbo la Igunga Kata ya Choma akiwa pamoja na Mmiliki wa kiwanda hicho, ndugu Urvesh Rajan pamoja na viongozi wa Serikali za mitaa, wahandisi na mafundi wa viwanda.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea na kuona maendeleo ya ufufuaji wa kiwanda hicho ili kianze kufanya kazi upya, baada ya kukaa kwa miaka kadhaa bila ya kufanya kazi, Mbunge Gulamali alisema, leo nimekuja kuoana maendeleo ya kufufuliwa wa kiwanda hichi ikiwa ni sehemu ya kutaka kutimiza tena ahadi yangu niliyo itoa kwa wanachi wa Igunga na Manonga kwamba lazima kiwanda cha Manonga Ginery, kianze kazi ili wananchi waweze kunufaika katika zao biashara ya pamba na wengine kupata ajira kwa kuendesha maisha na kukuza uchumi wa viwanda nchini.

" Leo nimekuja kuona maendeleo ya ufufuaji wa kiwanda hichi ikiwa ni sehemu yangu ya ahadi niliyo itoa kwa wananchi wangu wa jimbo la Manonga pamoja na Igunga kwamba lazima kiwanda hiki kifanye kazi tena, ili biashara ya zao la pamba lirudi tena na wananchi na waweze kupata ajira katika kiwanda hichi pia kukuza uchumi wa nchi ya Viwanda.

" Kufufuliwa kwa kiwanda hiki ni fursa kubwa ya maendeleo kwa jamii ya wana Igunga na Manonga na hasa wakulima wa zao la pamba hata kwa wananchi wanao lilia ajira, hivyo fursa kwa sasa iko wazi, alisema Gulamali.
 Mmiliki wa kiwanda cha Manonga Genery, Urvesh Rajan akizugumza na Mbunge wa Jimbo la Manonga, Seif Khamis Gulamali (katikati), alipotembelea kuona maendeleo ya ufufuaji wa kiwanda hicho jana Wilayani Igunga kata ya Choma. Kushoto ni Mwenyekiti wa Igombensabo Lazaro Ngullo .
 Mbunge wa Jimbo la Manonga, Seif Khamis Gulamali akipewa moja ya maelezo ya mashine ya ya zao la pamba ndani ya kiwanda cha Manonga Genery,jana alipotembelea kuona maendeleo ya ufufuaji wa kiwanda hicho kilichopo Wilayani Igunga kata Choma.
 Mmiliki wa kiwanda cha Manonga Genery, Urvesh Rajan akimpa maelekezo Mbunge wa Manonga Seif Khamis Gulamali ndani ya kiwanda hicho (katikati), jana alipotembelea na kuona maendeleo ya ufufuaji wa kiwanda kilichopo Wilaya ya Igunga kata ya Choma.
 Mbunge wa Jimbo la Manonga, Seif Khamis Gulamali (kushoto) akizungumza na Mwenyekiti wa Igombensabo.
 Mbunge wa Jimbo la Manonga, Seif Khamis Gulamali akiongozana na viongozi wa serikali pamoja na wahandisi alipotembelea kiwanda hicho jana kilichopo Wilayani Igunga kata ya Choma.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...