THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

MBUNGE NYALANDU ATANGAZA DONGE NONO KWA BINGWA WA KOMBE LA NYALANDU CUP

Na,Jumbe Ismailly SINGIDA July,03,2017 Nyalandu 


MBUNGE wa Jimbo la Singida Kaskazini,Lazaro Nyalandu ametangaza donge nono kwa timu itakayokuwa bingwa wa mashindano ya kombe la Mbunge huyo,maarufu kwa jina la “NYALANDU CUP” linalotarajia kuanza mwezi wa nane mwaka huu.

Kombe hilo litakaloanza mwezi ujao,litashirikisha timu za mpira wa miguu kwa wanaume na mpira wa miguu kwa wanawake na kilele cha mashindano ya kombe hilo kitafanyika katika Kijiji cha Ngamu,kilichopo katika Kata ya Mwasauya.

Akitangaza msimamo wake huo mbele ya Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka 2017,Amour Hamad Amour,Nyalandu alisema kwamba tangu alipochaguliwa kuwa mwakilisha wa wananchi wa jimbo hilo la Singida Kaskazini hajawahi kuandaa ligi ya aina yake kama hiyo inayotarajiwa kuanza kuchezwa katika jimbo zima.

“Nilimwambia Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru nafikiri nilikuwa namnong’oneza kwamba mwenge ukipita na hii itakuwa ni mara ya kwanza tangu nimekuwa Mbunge halafu kuchezesha mambo hii ya mechi”alifafanua ‘Mimi nafanyaaga maskolashipu,wasome sekondari,wafanye nini,mambo ya maji nafikiri sasa hivi tutaenda kwa zote, kwa hiyo ningependa kuanzisha ligi ambayo itafanyika ya mpira wa miguu lakini nataka iende sambamba na ligi ya wanawake” alisisitiza Mbunge Nyalandu.

Kwa mujibu wa Mbunge huyo kutakuwa na ligi ya wanaume na itafungwa pamoja na ligi ambayo itakuwa ni ya wanawake na ligi hiyo watashirikiana kuitangaza,kuiunda na kuiandaa na serikali ya wilaya hiyo pamoja na Halmashauri hiyo kwa ujumla.
Mchezaji wa timu ya Mtinko Fc,Yusufu Samsoni (mwenye jesi yenye rangi ya bluu) alipomtoka mchezaji wa timu ya Msange Fc,Yasini Athumani na kwenda kuifungia timu yake bao la pili na la ushindi.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya Msange FC wakifanya mazoezi katika uwanja wa michezo wa shule ya msingi Mtinko kabla ya kuanza kwa mchezo huo ambao matokeo yalikuwa Mtinko FC 2 na Msange FC 1.(Picha zote Na Jumbe Ismailly).