Na Ripota wa Mafoto Blog, Kibaha

MBUNGE wa Kibaha mjini, Silyvestry Koka (kulia) na Diwani wa Kata ya Sofu, Yusuf Mbonde, wakishirikiana na wananchi wa kata hiyo Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani, kusafisha eneo lililo na majani kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi wa Zahanati. Mhe. Mbunge leo asubuhi alifanya ziara ya kushitukiza katika eneo hilo baada ya kupata tetesi kuwa eneo hilo limeuzwa.

Aidha imeelezwa kuwa tetesi za kuuzwa kwa eneo hilo zilimfikia Diwani wa Kata hiyo, Bw.Mbonde, aliyeamua kumfuata Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji Kibaha, Jenifer Ommolo, ambaye 'eti' alikiri kuwa jambo hilo nalitambua na kumwahidi kuwa wangepewa eneo mbadala wa hilo, jambo ambalo Diwani hakukubariana nalo na kuamua kulifikisha kwa Mhe.Mbunge wake.

Mbunge huyo, alifika eneo hilo na kukutana na wapiga kura wake na kuamua kushiriki nao zoezi la kusafisha baada ya baadhi ya wananchi kukumbwa na hofu wakidai kuwa eneo hilo lilibadilishwa lengo la matumizi kwa kumgawia mtu aliyejulikana kwa jina la Mchome, ili kuliendeleza, ambaye pia hadi Mbunge anafika leo alikuwa bado hajaanza ujenzi wa aina yeyote.

Imeelezwa kuwa eneo hilo baada ya kutolewa kwa ajili ya kujengwa Zahanati ambayo kwa kiasi kikubwa ilitakiwa kujengwa kwa ushirikiano mkubwa na wananchi ambao wengi wao walipigwa na butwaa na kurudi nyuma baada ya kusikia eneo hilo amegaiwa Mchome, aliyetakiwa kuliendeleza.

Baada ya Mbunge Koka kuwasili eneo hilo hii leo asubuhi, wananchi wajitokeza na kuonyesha ushirikiano huo kwa kushirikiana na viongozi wao, na baadaye kubaki na matumaini ya kuona kinajengwa kile walichokikusudia baada ya Mbunge kutoa tamko kwa kusema eneo hilo linatakiwa kujengwa Zahanati ya wananchi na si kitu kingine.
Mbunge wa Kibaha mjini, Silyvestry Koka, akizungumza na wananchi wa Kata ya Sofu Wilayani Kibaha, wakati wa zoezi la kufyeka na kusafisha eneo la kujenga Zahanati,ambapo alilaani kitendo hicho cha uuzwaji wa eneo la wananchi alichokiita cha kitapeli.
Wananchi wakimsikiliza kwa makini mbunge wao, baada ya zoezi hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...