Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii


TIMU ya mpira wa Kikapu ya Mchenga Bball Stars imefanikiwa kuingia hatua ya fainali moja kwa moja baada ya kutoka na ushindi katika mchezo wa pili wa nusu fainali kwa kuinyuka Flying Dribblers vikapu 114 dhidi ya 52.

Katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Sprite Bball Kings 2017, Mchenga walifanikiwa kutoka na ushindi wa vikapu 119 dhidi ya 70 vya Flying Dribblers na kupelekea Mchenga kwenda hatua ya fainali baada ya kuibuka kidedea katika michezo miwil baina ya mitatu.

Michuano hiyo ya Sprite Bball Kings 2017 inayoendelea katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay ilizikutanisha timu nyingine katika mchezo wa pili wa nusu fainali baina ya Kurasini Heat dhidi ya TMT.

Kutokana na ushindi wa TMT wa mchezo wa pili kwa kuibuka kidedea kwa kuwabamiza Kurasini Heat vikapu 92 dhidi ya 61 huku katika mchezo wa kwanza Kurasini Heat wakiibuka kidedea kwa kushinda alama za vikapu 87 kwa 80.

Mchezo wa nusu fainali ya tatu ili kuweza kumpata mshindi atakayeungana na Mchenga katika hatua ya fainali, mchezo huo utapigwa siku ya Kesho katika Viwanja vya Don Bosco.

Fainali ya mchezo huo inatarajiwa kuanza siku ya Jumamosi katika Uwanja wa Ndani wa Taifa ikichezwa katika hatua tano ili kuweza kumpata bingwa wa Sprite Bball Kings 2017 na kuondoka na kitita cha Milion 10 huku mshindi wa pili akichukua Milion 3 na mchezaji bora wa Mashindano (MVP) akijinyakulia milion 2.

 Mpambano baina ya Mchenga (Nyeupe) dhidi ya Flying Dribblers (Bluu) ulimalizika kwa Mchenga kuingia katika hatua ya fainali baada ya kuibuka na ushindi aktika michezo miwili ya nusu faimali ikiwa inazisubiri timu za Kurasini Heat na TMT watakaovaana kesho katika fainali ya tatu Viwanja vya Don Bosco Oysterbay.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...