MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe. Isaya Mwita leo amefanya ziara ya kutembelea miradi ya Maendeleo ya jiji hilo ambapo ameridhishwa na vikundi vinavyotengeneza mkaa kwa kutumia malighafi ambapo amesema itasaidia kupunguza uchafu uliopo kwenye maeneo mbalimbali na kuliweka jiji katika hali ya usafi.
Ziara hiyo ambayo imehusisha Kamati ya Fedha ya Halmashauri ya Jiji, ilitembelea vikundi vya Maendeleo ya ujasiriamali cha Upendo Smart kilichopo mtaa wa Kilimahewa Kata ya Tandika kinachojihusisha na uzalishaji wa mkaa mbadala ( mkaa poa).
Aidha mbali na kikundi hicho Meya Mwita pia amejionea shuguli za uzalishaji wa mkaa unaofanywa na kikundi cha Maendeleo cha Mwangaza Vikoba kilichopo Pugu stesheni jijini hapa.
Akizungumza na wanakikundi hao, Meya Mwita amesema kuwa vikundi hivyo vinafanya kazi kubwa kutokana na ubunifu walionao jambo ambalo litasaidia kuweka jiji kwenye hali ya usafi. 

Jengo la mradi wa viwanda vidogo vidogo lililopo eneo la Karakana Mwananyamala jijini Dar es Salaam. Awamu ya kwanza ya jingo hilo limepangwa kutumia shilingi milioni 190, ambapo inatarajiwa mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu utakuwa umekamilika kwa asilimia 82.(Picha zote na Christina Mwagala, Ofisi ya Meya wa jiji) 
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita mwenye shati la kijivu akitoa maelekezo kwa maofisa Utumishi wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam leo alipofanya ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo ya jiji karakana ya Mwananyamala jijini hapa. 
Mhandisi katika Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Swalehe Nyenye akifafanua jambo kwa Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita alipofanya ziara ya kutembelea ujenzi wa viwanda vidogo Karakana ya Mwananyamala. 
Mkurugenzi wa kampuni ya Kuja na Kushoka tool Manufucture Leodard Kushoka akitoa maelezo jinsi namna ambavyo mashine ya kutengenezea nishati ya mkaa kwa kutumia malighafi inavyofanya kazi wakati wa ziara waliofanya kwenye kikundi hicho kilichopo Tandika. Wa kwanza kulia ni Diwani wa Kata ya Segerea Pratrick Asenga. 
Mashine inayotumika kutengeneza nishati ya mkaa 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...