Mwenyekiti wa kampuni ya Upimaji na Upangaji wa Makazi (HUSEA), Renny
Chiwa akitoa maelezo machache juu ya mradi wa 'Ardhi Clinic' katika
uzinduzi wa uliofanyika Kata ya Msigani-Mbezi wilaya ya Ubungo jijini
Dar es Salaam.
Bw. Chiwa alisema kuwa lengo la mradi huo ni kusaidia juhudi za serikali
za kupanga, kupima na kumilikisha kila kipande cha ardhi nchini nzima
na pia kuboresha maisha ya mamilioni ya watanzania kupitia ushauri na
utoaji elimu kwa wananchi katika masuala yote ya ardhu kwa nia ya
kutengeneza makazi bora yaliyopangwa na kupimwa kwa ajili ya kizazi cha
sasa na baadae.
Mkurugenzi
wa kampuni ya Upimaji na Upangaji wa Makazi (HUSEA), Pamela
Maro akiwafafanua machache mbele ya waandishi wa habari juu ya Mradi wa
'Ardhi Clinic' katika uzinduzi uliofanyika katika Kata ya Msigani, Mbezi
jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa malengo makuu ya mradi wa 'Ardhi Clinic' ni tiba mbadala
kwa changamoto mbali mbali za masuala ya ardhi baada ya kugundua kuwa
changamoto nyingi zinatokana na masuala ua ardhi hapa Tanzania kama
migogoro ya wafugaji na wakulima, wananchi kuuziwa maeneo ya wazi,
utapelikwenye masuala ya ardhi, uendelezaji wa makazi usiofuata mipango,
ukosefu wa maadili katika taaluma za upangaji na upimaji, ukosefu wa
hati miliki, ukosefu wa huduma za jamii n.k hazina tofauti na magonjwa
ambayo wanahitaji tiba haraka kuyakabili.
Wananchi wakiendelea kupata elimu ya ardhi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...