THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

MSUVA AAGA RASMI, YANGA WASHAMALIZANA NA DIFAA HASSAN ELJADIDI YA MOROCCO


Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano Yanga, Dismas Ten

Na Agness Francis, Globu ya Jamii.
Winga machachari wa timu ya Yanga Simon Msuva anatarajiwa kuondoka kuelekea nchini Morocco kwa ajili ya vipimo ili kujiunga na timu ya ya Difaa Hassani Eljadidi (DHJFC) inayoshiriki ligi kuu ya nchini humo.

Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano Yanga, Dismas Ten amesema kuwa mchezaji Saimon Msuva anatarajia kuondoka kuelekea nchini Morocco kwa ajili ya zoezi la vipimo vya afya ili kukamilisha mchakato katika timu ya Difaa Hassani Eljadidi (DHJFC).

Ten amesema walishamaliza mazungumzo na klabu hiyo kwa ajili ya kujiunga nao na wamempa baraka zote kijana wao kwa ajili ya kuanza maisha mapya ya soka nchini Morocco.
Timu hiyo ambayo  msimu uliopita  ilishikilia nafasi ya pili katika nmsimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 59, huku WCA Casablanca wakiwa kilelelni kwa point 66  katika ligi kuu ya Morocco inayojumuisha timu 16 kama ilivyo ligi kuu ya Tanzania bara. 

Hata hivyo uongozi wa Yanga unasubiri majibu ya vipimo vya Msuva na kuendelea na taratibu zote za kuuzwa kwa mchezaji huyo ambaye ameitumikia club hiyo misimu 5 akiwa kiungo mshambuliaji mwenye jezi namba 27.
Jana mchana  Msuva alikwenda klabu ya Yanga  kuaga na kupata baraka za viongozi wake waliokuwa nae katika maisha ya soka ndani ya Klabu ya Yanga kwa miaka mitano.