Mwenge wa Uhuru ukipelekwa eneo la mradi wa maji katika Kijiji cha Bukundi wilayani Meatu kwa ajili ya kufungua mradi huo.

Na Stella Kalinga, Simiyu

MWENGE wa Uhuru umeanza mbio zake rasmi leo katika mkoa wa Simiyu ambapo utapitia jumla ya miradi 43 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 8,450,841,622/=. Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka wakati akitoa salamu za Mkoa huo kwa Kiongozi wa kitaifa wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 , Ndg.AmourHamad Amour  katika kijiji cha Bukundi wilaya ya Meatu ukitokea katika mkoa Singida.

Mtaka amesema kati ya fedha hizo shilingi 680,285,524 zinatokana na Nguvu za wananchi ,Serikali Kuu shilingi 4,524,439,388, Halmashauri Shilingi 352,000,875, Washirika wa Maendeleo Shilingi 635,559,935 na Sekta binafsi Shilingi 2,258,555,900/=

Amesema Mwenge wa Uhuru utafungua miradi 14, kuzindua 13, kutembelea na kuona miradi 16 katika sekta ya Elimu,Afya,Maji,Vijana na wanawake, Miundombinu ya barabara, Sekta ya Viwanda, Maliasili, Kilimo, Ushirika na Utawala bora.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu , Mhe.Anthony Mtaka akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa moja wa wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa leo katika Kijiji cha Bukundi wilayani Meatu.

Aidha, Mtaka amesema katika kutekeleza kwa vitendo ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wa mwaka huu 2017 usemao “SHIRIKI KATIKA KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA KWA MAENDELEO YANCHI YETU”, Mkoa wa Simiyu umeweza kujipambanua katika utekelezaji wa Sera ya Tanzania ya Viwanda kupitia Kauli Mbiu ya “Wilaya Moja, Bidhaa Moja, Kiwanda Kimoja”

“Katika utekelezaji huu mkoa umefanikiwa kuanzisha kiwanda cha Chaki wilayani Maswa, Kiwanda cha Maziwa wilayani Meatu na Upembuzi yakinifu unaendelea mingine minne ambayo pia itatekelezwa katika Halmashauri zetu nyingine nne” Ameongeza katika miradi kuwa kukamilika kwa viwanda hivyo kutasaidia kutoa ajira kwa vijana wa mkoa wa Simiyu na mikoa jirani kutokana na kuwa malighafi zinazotumika na zitakazotumika katika viwanda hivyo zinazalishwa hapa nchini.

Naye kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru , Ndg. Amour Hamad Amour akifungua jengo la upasuaji kwa wanawake wajawazito katika kituo cha Afya Bukundi wilayani Meatu mbali na kuipongeza wilaya hiyo kwa kujali afya za wananchi wake hususani wanawake wajawazito pia alitaka mradi huo utunzwe na uthaminiwe.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akitoa salamuza Mkoa wakati wa kupokea Mwenge waUhuru kutoka Mkoani Singida katika kijiji cha Bukundi Wilayani Meatu.

“Mradi huu ni mzuri na mimi nimefurahi kuona naanza kuzindua miongoni mwa miradi inayogusa maisha ya wananchi moja kwa moja, hasa akinamama wajawazito hivyo basi nitoe wito kwa wanawake kutumia vizuri jengo hili badala ya kujifungulia majumbani hali inayoweza kuhatarisha afya zenu, vile vile mradi huu utunzwe na kuthaminiwa ili uendelee kutusaidia,”alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...