Na Robert Hokororo, Kishapu 
 Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 umepokelewa kimkoa kijiji cha Kinampanda kata ya Shagihilu katika wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga kutoka Simiyu na kuzindua miradi ya maendeleo yenye thamani ya sh. bilioni 3.7. 
Katika mapokezi hayo Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini alimkabidhi mwenzake wa Shinyanga, Albert Msovela ambaye alimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kishapu. 
Katika mbio hizo jumla ya miradi 12 ilizinduliwa ikiwemo ya kituo cha mafuta wenye thamani ya sh. milioni 337 kutoka kwa mjasiliamali Kija Ng’wani na mashine ya kusindika mafuta ya alizeti na unga wa mahindi sh. 244. 
Mingine ni mashine ya kukoboa mpunga na kuweka katika madaraja sh. milioni 535.8 na ufugaji ng’ombe sh. milioni 400 ya mjasiliamli Mabela Masolwa pamoja na eneo la viwanda lenye ekari 278 ambao thamani yake ni sh. bilioni 1.1.
Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela (kushoto) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa mwenzake wa Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini tayari kwa mbio hizo mkoani Shinyanga.
Mwenge wa Uhuru ukikimbizwa eneo la Maganzo wilayani Kishapu wakati ukiendelea kizindua miradi ya maendeleo. Kulia mbele ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga akitoa hamasa kwa wananchi. 
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa, Amour Hamad Amour akiweka nafaka ya mahindi katika mashine ya kusaga unga wakati wa uzinduzi wa mradi wa kiwanda kidogo cha kusindika alizeti na kusaga unga wakati wa mbio za Mwenge zilipopita kata ya Mwamalasa wilayani Kishapu mkoani Shinyanga jana.
Mwenyekiti wa halmashauari ya Kishapu, Boniphace Butondo akicheza ngoma wakati wa mapokezi ya Mwenge wa         Uhuru kijiji cha Kinampanda.
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa, Amour Hamad Amour akikagua bidhaa katika banda la wanawake wajasiliamali wilayani Kishapu eneo la mkesha Maganzo. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...