THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

NEWZ ALERT: MBUNGE HALIMA MDEE AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU KWA TUHUMA ZA KUMTUSI RAIS

Na Karama Kenyunko, blog ya jamii.

Mbunge wa Jimbo la Kawe kupitia Chadema, Halima amepandishwa katika kizimbani cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za kumtukana Rais Magufuli.

Halima Mdee amesomewa mashtaka yake na wakili mwandamizi wa Serikali, Nassoro Katuga mbele ya Hakimu Mkazi Victoria Nongwa.Imedaiwa, Julai 3, mwaka huu katika ofisi za Chadema zilizopo mtaa wa Ufipa Wilayani Kinondoni, jijini Dar es Salaam, alimtukana Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli, kuwa "anaongea hovyo anatakiwa afungwe breki".

Katuga aliongeza kudai kuwa, kitendo kile kingeweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Mdee anayetetewa na jopo la mawakili watano, likiongozwa na wakili Peter Kibatala amekana tuhuma hizo na yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana.Mahakama imemtaka Mdee kusaini ahadi ya sh. milioni 10 pamoja na wadhamini wawili ambao pia wamesaini ahadi ya kiasi hicho cha fedha.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika kwa kuwa bado wanasubiri taarifa muhimu za kisayansi, picha za video pamoja na maelezo ya mashahidi muhimu.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 7, mwaka huu.
 Mbunge wa Jimbo la Kawe Mhe. Halima mdee, akiwa amehifadhiwa katika ukumbi wa wazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salam leo akisubiri kusomewa kesi yake.

Mbunge wa Jimbo la Kawe Mhe. Halima mdee akisalimiana na Mbunge wa Bunda Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)  Mhe Esther Bulaya, akiwa amehifadhiwa katika ukumbi wa Wazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akisubiri kusomewa kesi yake.
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, atinga katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu tayari kwa kusikiliza tuhuma zinazomkabili mbunge wa jimbo la Kawe Halima Mdee. Picha ni Mbowe akisalimiana na Mdee