Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) lazindua utoaji wa mikopo kwa SACCOS na kupitia Benki ya Azania. Mikopo hii ni mahususi kwa ajili ya kuwasaidia wanachama wa NSSF kuweza kujikwamua kiuchumi hususan kuweza kutekeleza sera ya Viwanda ya awamu ya tano kwa kutumia mikopo hiyo kufungua Viwanda vidogo vidogo.

Mikopo hiyo itatolewa hadi kiwango cha juu kisichozidi fedha taslimu za kitanzania 300,000,000 kwa SACCOS au AMCOS. Vile vile mwanachama wa NSSF anaweza kukopa hadi shilingi 20,000,000 kupitia SACCOS au AMCOS aliyojiunga nayo na mikopo hiyo italipwa ndani ya miezi 24.

Alipokuwa akizindua mpango huo, Makamu wa Rais Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan aliwaasa wanachama wa NSSF kuchangamkia fursa hiyo ya mikopo na kuwaomba waitumie mikopo hiyo kama chachu ya kujikwamua kiuchumi na kuwaasa kuwa na nidhamu ya hali ya juu katika kuendeleza biashara zao.

Akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa mpango huo Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof Godius Kahyarara alisema SACCOS na AMCOS zote zitakaoomba mikopo hiyo ni lazima ziwasilishe taarifa sahihi za fedha zilizokaguliwa kwa miaka mitatu na kuhakikiwa na COASCO na mwanachama anaruhusiwa kukopa hadi mara tatu ya Amana zake alizijiwekea ndani ya SACCOS au AMCOS ambayo yeye ni mwanachama.
Makamu wa Rais wa Jammhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mikopo ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Kupitia Benki ya Azania alipotembelea banda la NSSF katika maonesho ya Sabasaba katika viwanja vya Mwalimu Nyerere.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kuhusu dawa ya kuangamiza viuadudu vinavyosababisha ugonjwa wa malaria alipotembelea banda la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) katika maonesho ya Sabasaba, viwanja vya Mwalimu Nyerere. NSSF ni mdau wa kiwanda hicho cha Viuadudu kilichopo mkoani Pwani.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara akitoa ufafanuzi kuhusu mikopo ya NSSF kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe Mama Samia Suluhu Hassan kabla ya  kuzindua rasmi mikopo hiyo katika viwanja vya Sabasaba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...