Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli, ameipongeza
Kampuni ya Simu Tanzania TTCL kwa juhudi kubwa inazofanya katika kuwapatia
Wananchi huduma bora za Mawasiliano.
Rais
Magufuli ametoa pongezi hizo baada ya kuitembelea Banda la TTCL katika Maonesho
ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam yanayoendelea.
Rais
Magufuli alitembelea TTCL mara baada ya kufungua rasmi maonesho hayo na
kukabidhi zawadi kwa Washindi ambapo TTCL iliibuka mshindi wa kwanza katika
kundi la Watoa huduma za Mawasiliano na Teknolojia
Katika
Banda la Maonesho la TTCL, Rais Magufuli alipokelewa na Mwenyekiti wa Bodi ya
TTCL Mhe Omari Nundu na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bw Waziri Kindamba
ambao walimhakikishia Mhe Rais kuwa TTCL inafanya mageuzi makubwa ya kibiashara
yatakayoiwezesha kurejea katika nafasi yake ya kuwa Kinara wa Sekta hiyo
nchini.
Kaimu
Afisa Mtendaji Mkuu TTCL Bw Waziri Kindamba alisema, anatarajia kuanza
kutoa gawio kwa Serikalini mwaka huu na kumuomba Mhe Rais kuiongezea
mtaji Kampuni hiyo ombi ambalo Mhe Rais alilipokea na kuahidi kulifanyia kazi.
|
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa
TTCL Bw Waziri Kindamba akipokea Tuzo ya mshindi wa Kwanza katika sekta ya
Mawasiliano na Teknolojia kutoka Mhe Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kwa, katika Viwanja vya Sabasaba .
|
|
1. Mhe Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akikaribishwa na wafanyakazi wa TTCL wakiongozwa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Mhe Omari Nundu na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bw. Waziri Kindamba, kwenye banda la TTCL katika Viwanja vya Sabasaba . |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo toka kwa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa
TTCL Bw Waziri Kindamba alipotembelea banda la shirika
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza kwa kazi nzuri Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bw Waziri Kindamba alipotembelea banda la kampuni
Mhe Dkt John Pombe
Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akitoka kwenye banda la TTCL
baada ya kutembelea banda hilo, katika Viwanja vya
Sabasaba
Wafanyakazi
wa TTCL wakiwa katika picha ya pamoja baada
ya kupata Tuzo ya Ushindi wa
Kwanza kwenye sekta ya
Mawasiliano na Teknolojia wa kiongonzwa na Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Mhe Omari
Nundu na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bw Waziri Kindamba, katika Viwanja
vya Sabasaba .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...