Serikali haijafuta mafunzo kwa watumishi wa umma ambapo Taasisi za Serikali zimeelekezwa kuandaa Mpango wa Mafunzo kwa watumishi kwa njia ya uwazi na shirikishi ili kuepuka malalamiko kutoka kwa baadhi ya watumishi wa umma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) amesema hayo leo katika kikao kazi na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, jijini Dar es Salaam.

Mhe. Kairuki amesema mwajiri anapoandaa Mpango wa Mafunzo kwa watumishi wake ni vyema mpango huo ukawa shirikisha kwa watumishi wote ili kujua mpangilio wake, ikiwa ni pamoja na kuandaa orodha ya ziada ya watumishi watakaochukua nafasi za wale waliopangwa kushiriki mafunzo lakini wakashindwa.

“Napokea malalamiko mengi sana kuhusiana na upendeleo katika suala la mafunzo, napenda kuwasisitiza waajiri tuandae Mpango wa Mafunzo ambao ni shirikishi kwa watumishi wote kuepuka haya, wengine wanapangwa na hawashiriki mafunzo,” Mhe. Kairuki amesema na kuongeza baadhi ya watumishi wa umma wanapangwa kushiriki mafunzo na hawaendi kwa sababu mbalimbali, lakini fursa ya nafasi hizo hawapangiwi wengine ili kuendana na mpango.

Mhe. Kairuki ameongeza kuwa Mpango wa Mafunzo shirikishi pamoja na kuondoa malalamiko, utasaidia pia kutorudisha fedha zilizobaki kwa watumishi wa umma ambao walipangwa lakini wakashindwa kuhudhuria mafunzo kwa sababu mbalimbali.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na viongozi na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala alipofanya ziara ya kikazi  katika Manispaa hiyo ili kupokea maoni, ushauri na kusikiliza kero za watumishi wa umma leo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Sophia Mjema akitoa hotuba ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) kuzungumza na watumishi wa umma katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Manispaa hiyo Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Bw, Msongela Palela akiwasilisha taarifa ya manispaa anayoiongoza kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) alipofanya ziara ya kikazi katika Manispaa hiyo ili kupokea maoni, ushauri na kusikiliza kero za watumishi wa umma leo Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (Hayupo pichani) wakati wa kikao kazi kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Mthibiti Mkuu Ubora wa Shule – Manispaa ya Ilala, Bi. Juliana Mhonyiwa akiwasilisha hoja wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha watumishi wa umma Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) leo Jijini Dar es Salaam.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...