Na Lorietha Laurence-WHUSM.

Serikali imeeleza kuwa inathamini na kutambua mchango mkubwa unaotolewa na Vyombo vya Habari nchini katika kuhakikisha kuwa jamii inapata taarifa sahihi na kwa wakati.

Akizungumza katika ziari yake alipotembelea vyombo vya habari vya Radio EFM na Radio One/ ITV leo Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel amesema kuwa lengo kubwa la Serikali ni kuwepo kwa ushirikiano mzuri na sekta ya habari nchini.

“Lengo la ziara hii ni kuimarisha uhusiano baina ya Serikali na vyombo vya habari pamoja na kufahamu utendaji wenu wa kazi na namna mnavyosimamia maudhui ya vipindi vyenu mnavyoviandaa” amesema Prof. Gabriel.

Aidha aliongeza kuwa ni jambo jema linalofanywa na watanzania wazawa kuwekeza katika sekta ya habari kwa kuwa dunia ya sasa imetawaliwa na utandawazi kupitia taarifa mbalimbali zinazotolewa zenye lengo la kuhabarisha na kujenga taifa letu. 

Kwa upande mwingine Prof. Gabriel amewataka watumishi wa vyombo hivyo vya habari kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, weledi na uzalendo ili kufikia malengo waliyojiwekea.Pia amewataka watumishi wa vyombo hivyo vya habari kujenga utamaduni wa kufanya kazi kwa kujituma ili kupata matokeo chanya katika soko la ushindani na kuifikia jamii kubwa zaidi katika kutoa habari za uhakikia na zenye usahihi.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiongea na watumishi wa Radio ya Efm (hawapo katika picha) alipofanya ziara ya kutembelea chombo hicho cha habari leo Jijini Dar es Salaam.
Watumishi wa Radio ya Efm wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (hayupo katika picha) alipotembelea chombo hicho cha habari leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Radio ya Efm pamoja na watendaji wa Wizara ya Habari wakati wa ziara yake leo Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) akiongea na Viongozi wa Radio One na ITV alipofanya ziara yake IPP Media leo Jijini Dar es Salaam kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji Radio One na ITV Bi. Joyce Mhaville.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (aliyekaa) pamoja na watendaji wa Wizara ya Habari wakiangalia namna mfumo wa urushwaji wa habari unavyofanya kazi katika studio za ITV wakati wa ziara yake leo Jijini Dar es Salaam.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...