THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

SERIKALI YAKEMEA UBOMOAJI WA MAJENGO YA KALE NCHINI

 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo amesema apendezi kabisa kuona shughuli za Ujenzi wa Majengo mapya zinaadhiri majengo ya kale bila sababu za msingi au kuridhiwa na Serikali.
 Akizungumza kwa niaba ya waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Dr Harson Mwakyembe, katika ufunguzi wa jengo la OLD BOMA lililopo jijini Dar es Salaam Naibu katibu Mkuu wa wizara hiyo Mh Nuru Milano amesema Sera ya Mambo ya kale ya mwaka 2007 inaimiza utunzaji wa majengo ya kale yenye zaidi ya miaka miamoja ili vizazi vilivyopo na vijavyo viweze kujifunza historia hii muhimu ya nchi yetu. 
Akitoa salama za Umoja wa nchi za Ulaya  Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya hapa nchini Mh Roeland Van De Geer wanesema Umoja huo unajisikia furaha kushiriki katika uhifadhi wa uridhi wa histori ya Tanzania hasa kwa kupitia majengo ya kale na kuahidi kuendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali katika uhifadhi huo. 
Nae Rais wa Wasanifu majengo nchini Mwandisi Henry. L.M. Mwoleka amewashau wananchi na taarisis mbali mbali kuacha kabisa kubomoa majengo ya kihistoria nchini ili kuendelea kuhifadhi majengo haya kama alama ya historia ya nchi yetu. 
Akitoa salama za shukrani Mea wa Jiji la Dar es Saalam Mh Isaya Mwita ameushukuru Umoja wa Nchi za Ulaya na wadau mbali mbali kwa kufadhili ukarabati wa jengo hilo la Kale na kuendelea kutoa wito kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kushiriki kikamilifu katika utunzaji wa Utamaduni huu wa Kihistoria kwani kwakufanya hivyo jiji la Dar es Salaam litaingiza mapato mengi kupitia Utalii.
 Naibu katibu Mkuu wa wizara hiyo Mh Nuru Milano (kulia) na Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya hapa nchini Mh Roeland Van De Geer wakifungua rasmi jengo la Kihistoria la Old Boma lililopo jiji Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa kituo cha Uridti wa Ubunifu Majengo Bi Aida Mulokozi  akitoa malezo ya onesho maalum lililopondani ya jengo la OLD BOMA, pembeni yake ni Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mh Isaya Mwita na wageni wengine wakimsikiliza kwa makini. 
 Wageni mbali mbali walioudhuria sherehe hizo za ufunguzi wakiangalia onesho maalum lililopondani ya jengo la OLD BOMA
Muonekano wa Jengo la kale la OLD BOMA lililopo eneo la Posta jijini  Dar es Salaam.