Tarehe 14 Julai, 2017 ilikuwa ni siku ya Tanzania Jijini Ottawa, Canada. Siku hii ilikuwa ni mwendelezo wa sherehe za kuazimisha miaka 150 ya uwepo wa Taifa la Canada. Mamlaka ya Jiji la Ottawa ilitoa fursa kwa ofisi mbalimbali za kibalozi kushiriki katika sherehe hizo ambazo zimekuwa zikiendelea tangu Januari 2017. Tarehe 14 Julai ilipangwa kwa ajili ya Tanzania.  Ubalozi wa Tanzania uliopo Jijini Ottawa ulitumia siku hiyo kuitangaza nchi yetu katika nyanja mbalimbali kama vile uchumi, utalii na utamaduni.

Balozi wa Tanzania nchini Canada Mhe. Jack Zoka akiwa na mkewe Bi. Esther Zoka, akikata utepe kuashiria kuanzishwa kwa shughuli mbalimbali zilizofanyika siku hiyo.

Bi. Petronilla Lyimo, Mshereheshaji wa siku hiyo ambaye ni mke wa Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Jumuiya ya Wana-diaspora wa Tanzania Jijini Ottawa (TAO)
Mhe. Balozi Jack Zoka akimtembeza Meya Jim Watson kwenye maonyesho ya vikundi mbalimbali vilivyoshiriki siku hiyo.
Afisa wa Ubalozi Bw. Leonce Bilauli akitoa zawadi kwa Meya wa Jiji la Ottawa Jim Watson alipotembelea ukumbi wa maonyesho akishuhudiwa na Balozi wa Tanzania nchini Canada Mhe. Jack Zoka.

 Afisa wa Balozi Bi. Aziza Bukuku akiwa kwenye banda la Ubalozi akielezea wageni kuhusu Tanzania. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...