TIMU ya Vijana wa Simba chini ya umri wa miaka 20, jana walishinda kuungana na wenzao wa Yanga katika fainali ya Mechi za Hisani kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI baada ya kufungwa na Tanzania Prisons kwa mikwaju ya penati 6-5 katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu wa Sokoine jijini Mbeya.

Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa timu zote kutoka uwanjani bila kupata bao, huku timu zote zikicheza kwa taadhari na kufanya mashambulizi ya kushitukiza.

Katika mchezo huo Simba ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 69 kupitia kwa mshambuliaji wake, Dadi Mbarouk, baada ya kuwatoka mabeki wa Tanzania Prisons Aron Kalambo, aliyekuwa ametoka golini akijaribu kuwahi kumzuia na  kupishana na mpira uliotinga wavuni.
Bao la kusawazisha la Tanzania Prisons, lilifungwa na Kassim Hamis, kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 79, baada ya mchezaji wa Simba U20, kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari na kufanya dakika 90 kumalizika timu hizo zikiwa sare kwa kufungana 1-1.

Baada ya sare hiyo timu hizo zilikwenda katika hatua ya matuta, ambapo zilipigwa jumla ya penati 8, na Tanzania Prisonswakikosa 2 na kupata penati 6 na Simba wakikosa 3 na kupata penati 5.

Simba wameungana na wenzao Mbeya City Kikosi cha kwanza ambao walitolewa na Kikosi cha Yanga U20 kwa kukubali kichapo cha mabao 3-0 katika mechi hizo za Hisani zilizoandaliwa na Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi Tanzania TACAIDS, na kushirikisha jumla ya timu Nne za Yanga U20 na Simba U20 kutoka jijini Dar es Salaam, Mbeya City na Tanzania Prisons vikosi vya kwanza Ligi Kuu Bara.
 Beki wa Simba U20, Jacob Jalala (kulia) akichuana kuwania mpira na mshambuliaji wa Tanzania Prisons, Mohamed Rashid, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa jana Julai 28, 2017 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Katika mchezo huo Tanzania Prisons ilishinda kwa mikwaju ya penati 6-5 baada ya mchezo huo kumalizka dakika 90 kwa sare ya 1-1. Picha na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
Beki wa Tanzania Prisons, Michael Ismail (kushoto) akijaribu kumpita mchezaji wa Simba U20, Rashid Juma, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa jana Julai 28, 2017 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Katika mchezo huo Tanzania Prisons ilishinda kwa mikwaju ya penati 6-5 baada ya mchezo huo kumalizka dakika 90 kwa sare ya 1-1.
 Beki wa Simba U20, Abdallah Rashid (kulia) akichuana kuwania mpira na mshambuliaji wa Tanzania Prisons, Kassim Hamis, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa jana Julai 28, 2017 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Katika mchezo huo Tanzania Prisons ilishinda kwa mikwaju ya penati 6-5 baada ya mchezo huo kumalizka  dakika 90 kwa sare ya 1-1.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...