Na Frank
Mvungi- Maelezo
Taasisi
ya Moyo ya Jakaya Kikwete imewataka Wananchi
kujitokeza kwa wingi kupima afya zao hasa magonjwa ya moyo katika msimu
huu wa maonesho ya Kimataifa ya 41 ya Biashara ya Dar es Salaam yanayofanyika
katika viwanja vya JK Nyerere jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
katika viwanja vya maonesho hayo Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi amesema kumekuwa
na muitikio mkubwa sana kwa wananchi kutembelea banda lao ambapo amesema kuwa kwa
siku takribani watu 700 wanafika katika banda hilo kwa ajili ya kupata huduma
na ushauri.
“Ni
vizuri watanzania wakatumia fursa hii kufika hapa na watapatiwa baadhi ya vipimo na
ushauri bure katika banda letu lililopo ndani ya viwanja vya sabasaba kwa
kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuwahudumia wananchi wake kwa
kuhakikisha kuwa wanapata huduma zote za msingi zenye kiwango na ubora,” Alisisitiza
Prof. Janabi
Akifafanua Prof. Janabi amesema Taasisi hiyo imedhamiria kuwahudumia wananchi
wakati wote wa maonesho na hata baada ya hapo wapo tayari kuwahudumia wale
wanaohitaji huduma katika taasisi hiyo.
Taasisi
ya Moyo ya Jakaya Kikwete imekuwa ikitoa huduma za upasuaji wa moyo tangu
kuanzishwa kwake hali inayosaidia kupunguza gharama zilizokuwa zinatumika
kusafirisha wagonjwa kwenda nje ya nchi kwa matibabu kwa kipindi kirefu sasa.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya
Kikwete (JKCI) Profesa Mohamed Janabi akiteta jambo na baadhi ya wafanyakazi wa
Taasisi yake alipotembelea Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara Dar es
Salaam leo. Kushoto ni Afisa Uhusiano wa Taasisi hiyo Bi. Anna Nkinda.
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo wa Taasisi ya
Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Bashir Nyangasa akielezea namna upasuaji wa
moyo unavyofanywa kwa mmoja wa mwananchi aliyetembelea banda la taasisi hiyo
katika Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) leo.
Wananchi wakipata huduma ya vipimo katika banda la Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF) leo.
Wananchi wakipata huduma ya vipimo katika banda la
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa Maonesho ya 41 ya Kimataifa
ya Biashara Dar es Salaam (DITF) leo. Picha na: Frank Shija – MAELEZO.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...