Na Ali O. Ali 
Kampuni ya Rafiki Network itafanya Tamasha la Michezo na Utamaduni linalojulikana kama “ Pemba Weekend Bonanza” litakalofanyika kisiwani Pemba kuanzia tarehe 28 hadi 30 Julai mwaka 2017. 
Taarifa ya kampuni hiyo imesema kwamba tamasha hilo litajumuisha matukio mbali mbali kama vile mchezo wa ng’ombe, resi za baiskeli, mashindano ya kuogelea na resi za ngalawa,  na kwamba miongoni mwa matukio, imeelezwa kwamba mchezo wa ng’ombe ambao utafanyika siku ya Ijumaa tarehe 28 Julai, 2017, majira ya alasiri katika viwanja vya skuli ya Chwale, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba. 
 Aidha, taarifa hiyo imebainisha kwamba resi za baiskeli ambazo zitafanyika kwa mizunguko miwili tafauti zitakuwa siku ya Jumamosi tarehe 29 na Jumapili tarehe 30 Julai katika maeneo na taratibu tofauti.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa, Siku ya Jumamosi, tarehe 29 Julai, kutakuwa na resi za baiskeli hatua ya mchujo, zitakazofanyika kwa kujumuisha makundi matatu yanayokimbia kwa kupitia barabara tatu tafauti kiswani Pemba. 
Fainali za resi za baisikeli zitaanzia Uwanja wa Gombani hadi Vumawimbi, Makangale Pemba majira ya saa 1 kamili asubuhi. 
Taarifa imethibitisha kuwa kutakuwa na mashindano ya kuogelea baharini yatakayofanyika siku ya Jumapili tarehe 30 Julai 2017 katika fukwe za Vumamwimbi. Shindano hili litawashirikisha waogeleaji mbalimbali nchini ambapo washiriki wapatao 100 watachuana katika mpambano huu. Vile vile taarifa hiyo imesema kwamba kutakuwa na resi za ngalawa zitakazofanyika tarehe 30 Julai, 2017, pia katika fukwe za Vumawimbi Pemba. Shindano litashirikisha ngalawa takribani 20 kutoka maeneno mbali mbali Kiswaini Pemba kama vile Tumbe, Kiuyu, Msuka, Shumba Mjini, Mwambe na Mnarani. Kwa mujibu wa taarifa hiyo Tamasha hili limedhaminiwa na ZURA (Zanzibar Utility Regulatory Authority) na litarushwa hewani na kituo cha Televisheni cha AZAM ambao ni washirika wenza (Partners) wa Kampuni ya Rafiki Network.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...