Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG )wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Prof Mussa J Assad wa pili kutoka kushoto akiwa na wajumbe wa Bodi ya Umoja wa Mataifa baada kikao cha 71 kinachoendelea mjini New York Marekani, kikao hicho kinafanyika kwa muda wa siku mbili.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu (CAG) za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Profesa Mussa Assad ambaye ni mjumbe wa Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa (UNBoA), jana tarehe 25 Julai, 2017 ameshiriki kuidhinisha ripoti za kaguzi za shughuli za Umoja wa Mataifa kwa mwaka ulioishia tarehe 31 Desemba 2016, kwenye kikao cha 71 cha Bodi ya Ukaguzi ya wanachama wa Umoja wa Mataifa kinachoendelea Mjini New York, nchini Marekani.

Katika kikao hicho, wajumbe wa bodi hiyo walipitia na kusaini ripoti ishirini na nane (28) za ukaguzi wa shughuli za Umoja wa Mataifa. Kati ya ripoti zilizoidhinishwa na wajumbe wa Bodi hiyo, ripoti kumi na moja (11) zilitokana na kaguzi zilizofanywa na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (NAOT) na kuwasilishwa na CAG, Prof. Mussa Assad kwenye kikao hicho cha Bodi. Aidha, ripoti kumi na saba (17) zilizosalia zilitokana na ukaguzi uliofanywa na Ofisi za Ukaguzi wa Hesabu za Serikali za India na Ujerumani.
Katibu Mkuu umoja wa Mataifa Bwana Antonic Guterres akizunguza na wajumbe wa Bodi ya Ukaguzi wa Umoja wa Taifa katika kikao cha Bodi kilichofanyika mjini New York Marekani hivi karibuni.

Ripoti kumi na moja zilizowasilishwa na Prof. Assad ni kaguzi za Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Shirika la Idadi ya Watu Duniani la Umoja wa Mataifa (UNFPA), Shirika la Ujenzi na Misaada la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wakimbizi wa Palestina na Mashariki (UNRWA), Mfuko wa Akiba kwa Watumishi wa UNRWA Wakazi (UNRWA – SPF), Shirika la Umoja wa Mataifa la Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji wa Wanawake (UN – Women), Mfuko wa Ukuzaji Mitaji la Umoja wa Mataifa (UNCDF), Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Makazi (UN Habitat), Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP), Mahakama ya Umoja wa Mataifa inayoshughulika na Mauaji yaliyotokea Rwanda (ICTR), Mahakama ya Umoja wa Mataifa inayoshughulika na Mauaji yaliyotokea Yugoslavia ya zamani (ICTY), Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kupunguza shughuli za mahakama za kimataifa (IRMCT).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...