THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

TIMU YA TANZANIA YASHIRIKI MASHINDANO YA ROBOTI NCHINI MAREKANI

Tarehe 16-18 Julai, 2017 Tanzania iliwakilishwa na Timu ya wanafunzi saba katika Mashindano ya Ubunifu yajulikayao kama First Global Robotic Challenge yaliyofanyika jijini Washington D.C

Timu hiyo iliongozwa na wakufunzi wawili, Bi. Mkufu Shaban Tindi na Bi. Carolyne Eryarisiima.

Tarehe 19 Julai, 2017 Timu hiyo ilitembelea Ofisi za Ubalozi wa Tanzaniani Washington, DC nchini Marekani kwa ajili ya kusalimia na kujitambulisha.