Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi, Arusha
Jeshi la Polisi mkoani hapa limefanikiwa kupunguza makosa ya jinai kwa mwaka huu 2017 toka 1,378 yaliyoripotiwa mwaka jana 2016 hadi kufikia 1,041 na kufanya idadi ya makosa yaliyopungua  kufikia 337. 
Akitoa takwimu hizo ofisini kwake  jana mchana, Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo (pichani), alisema kwamba punguzo hilo ni sawa na asilimia 24.4 huku akifafanua kwamba takwimu hizo ni kwa mujibu wa kuanzia mwezi  Januari hadi Juni mwaka huu 2017.
“Huu upungufu wa makosa ya jinai ni takwimu za nusu mwaka, toka Januari hadi Juni mwaka huu 2017 ikilinganishwa na mwaka 2016 kwa muda kama huo, hivyo utaona tumejitahidi “. Alifafanua Kamanda Mkumbo, huku akiendelea kubainisha.
“Mwaka jana kwa nusu mwaka makosa ya mauaji yalikuwa 45 lakini mwaka huu kwa kipindi kama hicho makosa yalikuwa 36 pungufu ya makosa 9, wakati makosa ya kubaka yalikuwa 106 kwa mwaka jana lakini mwaka huu yameshuka hadi kufikia makosa 79 pungufu ya makosa 27, huku makosa ya unyang’anyi wa kutumia silaha mwaka jana yalikuwa makosa 16 na mwaka huu kwa kipindi kama hicho yamekuwa makosa matatu sawa na upungufu wa makosa 13”. Alisema Kamanda Mkumbo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...