Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini Mhe. Hussein Mohammed Bashe ametoa ufadhili wa Masomo (Scholarship) kwa jumla ya wanafunzi 42 ndani ya Jimbo la Nzega Mjini ambao wamechaguliwa kujiunga na Masomo ya Kidato cha Tano kwenye  mikoa mbalimbali nchini.
Kabla ya hapo;  mwishoni mwa mwezi  Mei mwaka huu Mhe. Bashe aliwatunuku vijana hawa zawadi katika Tamasha kubwa la *Bashe Annual Academic Awards* ambapo kila mwanafunzi aliyefaulu kwa daraja la kwanza (Division One) alizawadiwa Pesa taslimu Tzs 100,000 huku wale waliopata Daraja la Pili (Division Two) walipatiwa Tzs 60,000 na wale wa daraja la Tatu walipatiwa Tzs 30,000 kwa pamoja na Counterbooks sita(6) kwa kila mwanafunzi kama sehemu ya pongezi na maandalizi yao ya shule; na leo hii amekamilisha kuwalipia ada za mwaka mzima watoto wote.
Hizi ni miongoni mwa jitihada za Mhe. Bashe katika kuwasaidia wadogo zetu na ndugu zetu ndani ya Jimbo la Nzega Mjini kuweza kufikia malengo yao katika Elimu na katika  maisha.
*Mhe. Hussein  Bashe*..... _"Ninafahamu fika kuwa Elimu ndio Ufunguo pekee na silaha muhimu katika maisha ya mwanadamu katika  vita dhidi ya Umasikini na Maradhi; nami nimeamua kuungana na Rais wangu *Dr. John Pombe Magufuli*  katika kuhakikisha tunawasaidia watoto wetu kuweza kupata haki ya msingi ya Elimu kwa ajili ya kuwa na taifa imara na kusaidia jamii nyingi masikini nchini."
Zoezi hili liliongozwa na Afisa Taaluma wa Halmashauri ya Mji wa Nzega Bw. Christopher Wilson Lusinde ambaye alifika kwa ajili ya kuwapongeza na kuwaaga vijana hawa huku akisindikizwa na Mwl. Saidi Uyaga kutoka Shule ya Sekondari Chief Ntinginya huku Ofisi ya Mbunge ikiwakilishwa na Bw. Godfrey Malema ambaye pia ni Afisa Mahusiano katika Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini.

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nzega Mjini
 Wanafunzi 42 ndani ya Jimbo la Nzega Mjini ambao wamechaguliwa kujiunga na Masomo ya Kidato cha Tano kwenye  mikoa mbalimbali nchini.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...