Ujenzi wa Daraja la Kavuu lenye urefu wa Mita 89 linalounganisha Halmashauri ya Wilaya ya Mlele na Halmashauri ya Wilaya ya Mpwimbwe Mkoani Katavi ujenzi wake umekamilika na litaanza kutumika ifikapo mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu.

Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa Daraja hilo Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani amesema kukamilika kwa ujenzi huo kutarahisisha usafirishaji wa abiria na Mizigo kutoka Mkoa wa katavi kwenda mikoa ya jirani.

“Serikali iliona kero kubwa wanazozipata wananchi wa mkoa huu hasa kwenye usafirishaji wa abiria na mizigo kwenye kipindi cha mavuno, hivyo baada ya kukamilisha Daraja hili wananchi wataweza kupita vipindi vyote vya Mwaka,” alisema Naibu Waziri Eng. Ngonyani.

Aidha, Eng. Ngonyani amemuagiza Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Katavi Eng. Abdon Maregesi Kuhakikisha Mzani unaohamishika unawekwa ili kudhibiti magari yatakayozidisha Tani 36.

Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoa wa Katavi Eng. Abdon Maregesi amemuhakikisha Naibu Waziri, Eng. Ngonyani kuwa wakala utaweka mzani huo ili kutoruhusu magari yaliyozidisha Uzito wa Mzigo kupita kwenye Daraja hilo.
 Naibu Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Wa kwanza kushoto), akikagua ujenzi wa Nyumba za viongozi zinazojengwa na Wakala Wa Majengo nchini (TBA) Mkoani Katavi, Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Mlele Bi. Rachel Kassanda.

 Meneja Wa Wakala Wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Abdon Maregesi (kulia), akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Katikati) juu ya hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa Daraja la Kivuu wakati Naibu Waziri huyo alipokagua, Mkoani Katavi.

 Muonekano wa Daraja la Kavuu lenye urefu wa Mita 89 linalounganisha Halmashauri ya  Wilaya ya Mlele na Halmashauri ya Wilaya ya Mpwimbwe Mkoani Katavi ambalo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 99.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...