THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Ujumbe Ubalozi wa Israel Watembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili Leo

 Ujumbe kutoka Ubalozi wa Israel nchini Kenya umetembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo. Maestro Nir Brand akipiga kinanda ili kuwaburudisha watoto wanaopatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Kushoto ni Ofisa Uhusiano kutoka ubalozi huo, Angela Mogusu.  
 Watoto wanaotibiwa katika hospitali hiyo wakisikiliza moja wa wimbo uliokuwa ikiimbwa na Brand leo kwenye Jengo la watoto.
 Watoto wakicheza na Daktari Bingwa wa Watoto, Rehema Laiti leo.
  Ilala Brand akipiga makofi ikiwa ni sehemu ya kuungana wagonjwa leo. Dk. Shlomi Cohen akishiriki katika shughuli ya kuimba na kucheza na watoto hao leo.


Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.

  1. Mbele Anasema:

    Ankal,

    Za masiku? Nimevutiwa na hii taarifa. Nimejifunza na kujione huku ughaibuni kuwa siku hizi wanatambua na kutumia sanaa kwa namna mbali mbali ikiwmo katika matibabu. Kuna dhana kama "art therapy" na hii inayoelezwa katika taarifa yako huitwa "music therapy." Hii "art therapy" inajumlisha pia burudani ya hadithi.

    Katika kutafakari suala hili, nimetambua kuwa wale waganga wetu wa enzi za wahenga walikuwa wanafanya sawa walipokuwa wanaimba, au wanapiga ngoma na ala zingine za muziki katika aina fulani fulani za matibabu. Wazungu walikosea walipopuuza jadi zetu hizi na kuziita za kishenzi. Ila sasa, kama nilivyotamka hapa juu, nao wameamka usingizini.