Na Sekela Mwasubila. Afisa habari Ulanga
Katibu Tawala Msaidizi Bw. Noel Kazimoto ametoa pongezi hizo wakati wa ziara yake ya ukaguzi na uhamasishaji na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo ndani ya wilaya akiwa na viongozi kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI. 
 Bw. Kazimoto aliwapongeza viongozi wa kijiji hicho na watu wote waliochangia ujenzi huo hadi hatua hiyo na kuwakumbusha kusoma mapato na matumizi ya ujenzi huo na kuwashauri kuendelea kubuni miradi yenye manufaa kwa wananchi. 
 Hata hivyo Bw. Kazimoto aliwataka wakuu wa Idara kusimamia miradi yote ndani ya wilaya na kufanya ufuatiliaji katika ngazi za chini ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma stahiki na kwa wakati. 
 Akitoa taarifa ya ujenzi wa ofisi ya kijiji cha Safari Road Afisa Mtendaji wa Kijiji Bi. Sophia Haule amesema kuwa ujenzi huo uliibuliwa na wananchi na viongozi kutokana na kukosekana kwa ofisi ya kijiji na kuwalazimu kupanga ofisi ambayo ni finyu na gharama. 
Aliongeza kuwa ujenzi umefanikiwa kutokana na msaada wa nguvu za wananchi, fedha za Halmashauri na fedha za mfuko wa jimbo ambapo hatua iliyofikia ni umaliziaji na uwekaji wa samani. 
 Ziara ya ufuatiliaji wa miradi imefanyika wilayani Ulanga na mkoa kwa ujumla ikihusisha viongozi kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI na ofisi ya Katibu Tawala Mkoa ambapo kwa wilaya ya Ulanga walitembelea miradi ya ujenzi wa vyoo shule ya Msingi Mahenge Mjini, ujenzi wa soko la Kijiji cha Mahenge, maabara shule ya sekondari Mahenge na ujenzi wa Ofisi ya Kijiji cha Safari Road.

Bibi Beatrice Msomisi kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI akikagua jengo la ofisi ya Kijiji cha Safari Road iliyopo katika kata ya Mahenge Mjini alipofanya ziara ya ukaguzi wa miradi wilayani hivi karibuni.
Wakuu wa Idara wa Halmashauri Ya wilaya ya Ulanga wakiwasikiliza kwa umakini watumishi kutoka Ofisi ya Katibu Tawala Morogoro na Ofisi ya Rais TAMISEMI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...