THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Viane Kundi wa Iringa ajishindia Milioni 20 za Biko*Issa naye achota Mil 10 zake.

Na Mwandishi Wetu, Dar es SalaamBAHATI Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’ imezidi kushika kasi baada ya droo yake ya 27 kutua kwa Viane Kundi wa mjini Iringa, nchini Tanzania aliyevuna jumla ya Sh Milioni 20, huku Ally Issa Kumburu mkazi wa Mwananyamala, jijini Dar es Salaam naye akivuna Sh Milioni 10 za Tamasha la Komaa Concert, lililofanyika jana na kudhaminiwa kwa kiasi kikubwa na Biko.

Droo zote mbili zilichezeshwa leo jijini Dar es Salaam kwa kuendeshwa na Balozi wa Biko, Kajala Masanja na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Emmanuel Ndaki, ambapo ni matokeo ya kutopatikana kwa mshindi wa tamasha la Komaa Concert, lililofanyika juzi katika Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika droo hiyo ya 27, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kupatikana kwa washindi hao ni sehemu ya kuendelea kugawa fedha kwa kwa wote wanaoshinda katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, akiwamo Kumburu wa Komaa Concert, mkazi wa Mwananyamala, jijini Dar es Salaam na Viane aliyejinyakulia Sh Milioni 20 akitokea mkoani Iringa.Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Emmanuel Ndaki, kushoto akiandika dondoo katika droo ya Komaa Concert iliyorudiwa leo asubuhi baada ya jana kutopaatikana mshindi katika Tamasha la Komaa lililoandaliwa na EFM Radio na kudhaminiwa na Bahati Nasibu ya Biko Tanzania. Kulia ni Balozi wa Biko, Kajala Masanja.
Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Emmanuel Ndaki, kushoto akiandika dondoo katika droo ya 27 ya Biko ambapo Viane Kundi wa Iringa, alitangazwa mshindi na kuzoa Sh Milioni 20 za Biko. Kulia ni Balozi wa Biko, Kajala Masanja.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa Paulo Makonda, akizungumza na wadau wa muziki waliofurika katika Tamasha la Komaa Concert lililoandaliwa na EFM Radio kwa udhamini mkubwa wa Bahati Nasibu ya Biko 'Ijue Nguvu ya Buku'. Katika Tamasha hilo lililokwenda na kumpata mshindi wa Sh Milioni 10 limempata Ally Issa Kumburu wa Mwananyamala, aliyepatikana katika droo iliyochezeshwa leo baada ya ndani ya tamasha kutopokea simu kutokana na wingi wa watu na kelele za uwanjani Tanganyika Packers, Kawe. Mwingine pichani ni Mkurugenzi wa EFM Radio, Denis Busurwa (Sebo). Picha na Mpigapicha Wetu.