Asasi za Kiraia za zinazounda Umoja wa AZAKI za juu ya masuala ya Bunge kwa kushirikiana na asasi zingine waja na mapendekezo katika kuboresha Sera ya Taifa ya Vijana ya mwaka 2007 ili iendane na wakati pamoja na mabadiliko ya kiteknolojia.
Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana Tanzania (TYVA) ambayo ni Asasi kiongozi Bw. Suleiman Makwita wakati akiwasilisha muhtasari wa uchambuzi wa Sera hiyo.
Makwita amesema kuwa lengo la kufanya mapitio juu ya Sera hiyo ni kuangalia namma ambapo wanaweza wakaishauri Serikali maeneo ya kufanyia maboresho katika Sera hiyo ya vijana.
“lengo la kufanya uchambuzi huu ni kuiomba Serikali na wadau wote wa maendeleo ya vijan nchini kuweka mazingira rafiki yatakayochochea maeneleo ya vijana kupitia sekta rasmi na zisizo rasmi ikijuisha masuala mtambuka na kuendana na dhana ya maelengo endelevu ya dunia” alisema Makwita.
Akizungumzia matokeo ya uchambuzi huo Makweta alisema kuwa wamebaini baadhi ya changamoto zilizopo katika Sera ya Vijana ya Mwaka 207 na hatimaye wamekuja na baadhi ya mapendekezo kama njia ya kusaidia kuiboresha Sera hiyo.
Baadhi ya mapendekezo waliyokuja nayo ni pamoja na kuanishwa kwa umri wa kijana kuwa miaka 13 -35 tofauti na sasa ambapo kijana anatambuli kuwa na umri kati ya 15 hadi 35.
Aliongeza kuwa katika masuala ya afya Sera inapaswa kukugusia masuala yote yanayoathiri vijana kama vile afya ya uzazi, anemia,TB na Selimundu, badala ya kutilia mkazo kwenye VVU/Ukimwi pekee.
Pamoja na mapendekezo hayo Makwita aliipongeza Serikali kwa juhudi zake za kuendelea kuweka mazingira rafiki kwa vijana kijana, pamoja nakufanyia kazi baadhi ya mapendekezo ya wadau mbalimbali ikiwemo kuanzishwa kwa Baraza la Taifa la Vijana.
Uchambuzi huu wa Sera ya Taifa ya Vijana ya Mwaka 2007 umefanywa kwa ushirikiano baina ya umoja wa AZAKI za Vijana juu ya Masuala ya Bunge na Mtandao wa AZAKI za Vijana juu ya Masuala ya Afya ya Uzazi chini ya uongozi wa Asasi ya Dray a Vijana Tanzania (TYVA).
Mwenyekiti wa Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana Tanzania (TYVA) Bw. Suleiman Makwita akiwasilisha muhtasari wa uchambuzi wa Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana  ya mwaka 2007 mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) akiwa pamoja na baadhi ya wananchama wa asasi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. 
 Mwenyekiti wa Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana Tanzania (TYVA) Bw. Suleiman Makwita akiwasilisha muhtasari wa uchambuzi wa Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana  ya mwaka 2007 mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) akiwa pamoja na baadhi ya wananchama wa asasi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. 
Wanachama wa Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana Tanzania (TYVA) wakiwa katika pica ya pamoja mara baada ya kumaliza kuwasilisha muhtasari wa uchambuzi wa Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana  ya mwaka 2007 kwa waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...