Benny Mwaipaja, WFM
Wizara ya Fedha na Mipango imetiliana saini na Kampuni ya ujenzi wa barabara ya Reynolds kandarasi ya ujenzi wa barabara ya kutoka Kidatu hadi Ifakara mkoani Morogoro, yenye urefu wa kilometa 67 kwa kiwango cha lami utakaojengwa kwa shilingi bilioni 101, kupitia ufadhili wa Umoja wa Ulaya, Marekani na Uingereza. 


Mkataba huo umesainiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Shaaban kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Bw. Dan Yzhak Shahn, Bw. Benjamin Arbit ambaye ni Mkandarasi kutoka Kampuni ya Ujenzi ya Reynolds. 


Kiasi hicho cha fedha ni sawa na Euro milioni 40.4 ambapo Euro milioni 29.6 zimetolewa kwa ushirikiano wa Umoja wa Ulaya na Shirika la Misaada la Uingereza-UK-AID, huku kiasi kinachobaki cha Euro milioni 10.8 kikitolewa na Shirika la Misaada la watu wa Marekani- USAID. 


Akizungumza mara baada ya kutiwa saini kwa kandarasi hiyo, Bi. Amina Khamis Shaaban, amesema ujenzi wa barabara hiyo utakaohusisha pia ujenzi wa daraja katika Mto Ruaha Mkuu, utasaidia wakulima wadogo kupitia Program ya Uendelezaji Kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania-SAGCOT, walioko katika Bonde la Mto Kilombero, kuyafikia masoko ya uhakika ya mazao yao.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban (wa pili kulia) na Mkandarasi kutoka Kampuni ya Ujenzi ya Reynolds, Bw. Dan Yzhak Shahn (kushoto) wakisaini mkataba wa Sh. Bilioni 101 kwa ajili ya ujenzi wa Barabara ya Kidatu- Ifakara yenye urefu wa Kilometa 66.9, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam. 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban (kulia) na Mkandarasi kutoka Kampuni ya Ujenzi ya Reynolds, Bw. Dan Yzhak Shahn (kushoto) wakibadilishana mkataba wa Sh. bilioni 101 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Kidatu – Ifakara yenye urefu wa Kilometa 66.9, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam. 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban (kushoto) akizungumza kuhusu umuhimu wa barabara ya Kidatu – Ifakara kwa kiwango cha lami kwa maendeleo ya Kilimo baada ya kutiliana saini mkandarasi atakayejenga barabara hiyo, hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam. 
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Tanzania, Roeland van de Geer akizungumza kwa niaba ya EU, UK-AID na USAID, kuhusu mpango wao wa kuendelea kuisaidia Tanzania katika ujenzi wa miundombinu baada ya kuwekwa saini mkataba wa Sh. bilioni 101 kwa ajili ya Ujenzi wa barabara ya Kidatu – Ifakara, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban. 
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria hafla ya kuwekwa saini mkataba wa Sh. bilioni 101 kwa ajili ya Ujenzi wa barabara ya Kidatu – Ifakara wakifuatilia nyaraka za mkataba huo kabla ya kusainiwa, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM) 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...