Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

MASHINDANO ya European Youth Film 2017 imewatangaza washiriki 15 waliofanikiwa kuingia hatua hiyo baada ya kutengeneza filamu fupi zenye maudhui tofauti.

Shindano hilo liliwashirikisha washiriki zaidi ya 120 na kuwachuja na kufikia 35 na tayari wamewapata washiriki 15 walioingia katika
kinyang'anyiro hicho na maamuzi yatakuwa mikononi mwa wananchi.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa utangazaji wa washiriki hao, Balozi wa Umoja wa Ulaya Roeland Van De Geer amesema kuwa wameziangalia filamu hizo katika maudhui tofauti na wamechujwa kwa kushirikiana na Bodi ya Filamu nchini.
Balozi wa Umoja wa Ulaya Roeland Van De Geer akizungumza na waandishi wa habari wakati wa utangazaji wa washiriki 15 waliofanikiwa kuingia hatua hiyo baada ya kutengeneza filamu fupi zenye maudhui tofauti.Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Huduma za Ufundi wa Bodi ya Filamu Wilhad Tairo na Kulia ni Afisa wa habari wa Umoja wa Ulaya Sussane Mbise.
Kaimu Mkuu wa Huduma za Ufundi wa Bodi ya Filamu Wilhad Tairo akuzungumza na kuupongeza Umoja wa Ulaya kwa mashindano waliyoaanzisha ya kuibua vipaji kwa waandaaji wadogo wa Filamu nchini, kushoto ni Mratibu wa mashindano Mussa Sakala.

De Geer amesema kuwa, filamu hizo 15 zitaoneshwa katika maeneo ya wazi ndani ya Jiji la Dar es salaam kwenye Viwanja vya Biafra Agost 5, Zakhem Agosti 12, Mwembe Yanga Agosti 19 na ukimbi wa Alliance Francais Septemba 02 ambapo washiriki watano wataingia hatua ya fainali.

Kaimu Mkuu wa Huduma za Ufundi wa Bodi ya Filamu Wilhad Tairo amesema kuwa mashindano haya yana tija kubwa sana katika kuibua vipaji ya sanaa na zaidi lazima tuanze kuangalia kutoka chini ili kupata waandaaji wapya na wenye ubunifu katika sekta ya sanaa hususani Filamu.

Mashindano hayo yatafikia tamati mwezi Septemba mwaka huu na yanaratibiwa na Umoja wa Ulaya nchini Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...