Na Tiganya Vincent-RS-TABORA

Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Dkt. Thea Ntara amemtaka Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Kitete kuwakama mara moja na kuwafikisha Polisi watumishi wawili wa Hospitali hiyo wanaotuhumiwa kukutwa na dawa na vifaa tiba katika mikoba yao.

Dkt. Ntara alitoa kauli hiyo jana(leo) mjini Tabora baada ya watumishi hao kukamatwa na vifaa hivyo katika mikoba yao kinyume na utaratibu wa hospitali na ambazo dawa hizo na vifaa wanatuhumiwa walikuwa wakitaka kwenda kuziuza katika hospitali binafsi.

Alisema kuwa baada ya kukamatwa na kupekuliwa katika mikoba yao ndipo walikuwa na dawa na vifaa tiba ambavyo havitakiwa kutoka nje ya hospitali na havikuwa na maelekezo ya Mganga.Kufuatia kazi hiyo ilifanywa na walinzi hao Katibu Tawala huyo wa Mkoa aliwapongeza na kuwaagiza kuongeza kupekua watu wote wanaokwenda kuona wagonjwa kwa sababu yawezekana watumishi wengine ambao sio waadilifu wakatumia nafasi hiyo kutorosha dawa na vifaa tiba.

Alimwagiza Mganga Mfawaidhi wa Hospitali hiyo kuhakikisha watuhumiwa hao wanakamatwa mara moja na kufikishwa Polisi wakati hatua nyingine za kiutumishi zinaendelea.Watumishi waliokamatwa kwa tuhuma za kukutwa na dawa na vifaa tiba katika mikoba yao ni Petronila Mbipa Bundala ambaye ni Mhudumu na Monica Alexanda Rugeinamu ambaye ni Muuguzi.

Aidha ameagiza watumishi hao waandikiwe mara moja barua za kusimamishwa kazi kutokana na tuhuma za kukutwa na mali ya mwajiri wao kinyume na sheria.Vifaa na dawa vilivyokamatwa ni Cannula, Surgical gloves, Syringesa, Urinal bag, IV giving set, Blood giving set,Brainded silk number, water injection, powder, soap, examination grolve, gentamyacin injection ampule, ascorbic acid.

Hivi karibuni Hospitali hiyo imekumbana na wizi wa mara kwa mara hatua iliyopelekea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora kusimamisha Kampuni iliyokuwa imepewa jukumu la kulinda na kulazimika kuweka Kampuni nyingine wakati taratibu za kuichukulia hatua Kampuni ya awali zikiendelea.

Kuanza kwa Kampuni mpya tayari watuhumiwa hao wamekamatwa na ulinzi umeimarishwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...