THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Waziri Dkt. Mwakyembe aunda Kamati ya Watu 10 kujadili sakata la TBC na Kampuni ya Star Times.

Na Lorietha Laurence -WHSUM.

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ameunda kamati ya wajumbe 10 kwa ajili ya kufuatilia undani wa kutopatikana kwa faida kati ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na kampuni ya Star Times kutoka China.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam alisema kuwa kamati hiyo imepewa siku saba kuhakikisha inakuja na taarifa kamili kuhusiana na suala hilo.

“ nimeipa kamati hii muda wa siku saba ukimalizika siiongezi tena nitatoa labda siku moja mbili kumalizia tu ili inipatie majibu kamili kwa nini kwa miaka yote hiyo hakuna faida”alisema Mwakyembe.

Aidha Dkt. Mwakyemba anaeleza kuwa uamuzi wa kuunda kamati hiyo ni kutokana na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuonyesha kukerwa na kutokupatikana kwa faida kwenye ushirikiano huo wa TBC na Star Times alipofanya ziara yake mwezi Mei mwaka huu.

Anazidi kufafanua kuwa Rais alikasirishwa na kitendo cha kampuni hiyo kufanya kazi nchini kwa kipindi cha miaka saba bila faida yoyote na hivyo kuagiza hatua stahiki kuchukuliwa juu ya suala hilo.

Dkt. Mwakyembe anabainisha kuwa tangu kutolewa kwa kauli ya Rais Mhe. Dkt. Magufuli Wizara na watendaji wake tayari wameshafanya mikutano miwili mmoja Mjini Dodoma na mwingine Jijini Dar es Salaam wakajadili kwa kina sababu zinazopelekea kushindwa kupatikana kwa faida.

Kabla ya mkutano na waandishi wa habari ,Waziri Dkt. Mwakyembe alitumia takribani saa tatu akijadiliana kwa kina na Mwenyekiti wa Kampuni ya Star Times kutokea nchini China, Xinxing Pang pamoja na wafanyakazi wa wizara akiwamo Katibu Mkuu Profesa Elisante Ole Gabriel na Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo, Dkt.Hassan Abbas.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Star Times Bw. Xinxing Pang alisema kuwa ana imani kuna uwezekano wa kumalizwa kwa suala hilo kwa kutumia wataalamu wake watakaoangalia sababu za kutokupatikana kwa faida na nini kifanyike katika kuondokana na changamoto hiyo.
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiongea na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Katibu Mkuu kutoka Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel na kulia ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Star Times Bw. Xinxing Pang.
Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo katika picha) alipokuwa akieleza msimamo wa Serikali kuhusiana na Kampuni ya Star Times jana Jijini Dar es Salaam. (Picha na Lorietha Laurence.)