Waziri Ummy Mwalimu akihutubia kwenye mkutano huo ambapo aliwasisitiza watoa huduma za afya kote nchini kuweka malengo ya kuwagundua wahisiwa wote takribani laki moja ambao hawajafikiwa ili kuweza kuwakinga watanzania wasipate maambukizi ya kifua kikuu (TB).
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy mwalimu akibadilishana mawazo na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohamad Bakari Kambi(kushoto) na Meneja Mpango wa Taifa wa kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma dkt. Beatrice Motayoba (kulia) kabla ya Ufunguzi wa Mkutano huo uliofanyika kwenye Hoteli ya Kilimani Landmark Mjini Dodoma
Baadhi ya waratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma toka Mikoa mbalimbali wakifuatilia hotuba ya Mhe.Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto(hayupo pichani)
Mwakilishi wa Mfuko wa Fedha wa Dunia (Global Fund ) toka Geneva dkt.Osamu Kunii akiongea na waratibu walioshiriki mkutano huo ambapo alisema Tanzania ni nchi ya pili kwa kupata ufadhili mkubwa katika Bara la Afrika ikitangaliwa na Nigeria
Waziri Ummy Mwalimu akifurahia jambo na Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani nchini Tanzania Dkt. Richard Banda (kulia) wakati wa mkutano huo,kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof.Kambi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...