THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Waziri wa usalama wa Kenya Jenerali Mstaafu Joseph Nkaissery afariki dunia.
Jenerali Joseph Ole Nkaissery enzi za Uhai wake.
 
Waziri huyo amefariki dunia saa chache baada yake kulazwa katika hospitali ya kibinafsi ya Karen kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu. 
Taarifa za kifo chake zimetangazwa na mkuu wa utumishi wa umma Bw Joseph Kinyua mwendo wa saa kumi na moja alfajiri. 

“Ni kwa huzuni kubwa na mshangao kwamba tunatangaza kifo cha ghafla cha Waziri wa Usalama wa Ndani Jenerali Mstaafu Joseph Nkaissery,” taarifa ya Bw Kinyua imesema. 

“Taifa litaendelea kupashwa habari zaidi punde maelezo yatakapopatikana.”
Jenerali Nkaissery amefariki siku chache baada ya mwanasiasa mkongwe G.G Gitahi aliyekuwa seneta wa jimbo la Laikipia kufariki dunia.

Waziri wa elimu nchini Kenya Dkt Fred Matiang'i (pichani) ameteuliwa kuwa kaimu waziri wa usalama wa ndani kufuatia kifo cha aliyekuwa waziri Meja Jenerali Mstaafu Joseph Nkaissery.