Mkuu wa Wilaya ya Geita Herman Kapufi akizungumza wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa maofisa ugani wa wilayani yake wilayani humo jana yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), yenye lengo la kuwakumbusha wataalamu hao wa kilimo nafasi yao pamoja na kuwapatia mbinu mpya za kisasa katika kulima mazao ya Mihogo, Pamba na Viazi vitamu katika kuelekea serikali ya viwanda.

Na Dotto Mwaibale, Geita

HALMASHAURI ya Wilaya ya Geita Mkoani Geita imesema itahakikisha inatenga bajeti ya shilingi milioni 50 kuwezesha mafunzo na kuboresha sekta ya kilimo kutoka kwenye fedha zake pamoja nakuwaomba wadau wengine wa wilaya kama vileKampuni ya uchimbaji dhahabu ya geita GGM kuchangia milioni 200 ili kuinua sekta hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya hiyo, Herman Clement Kapufi wilayani humo jana wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa maofisa ugani wote wa wilayani yake yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), yenye lengo la kuwakumbusha wataalamu hao wa kilimo nafasi yao pamoja na kuwapatia mbinu mpya za kisasa katika kulima mazao ya Mihogo, Pamba na Viazi vitamu katika kuelekea serikali ya viwanda.
Maofisa ugani wakiwa kwenye mafunzo hayo.

Mkuu huyo wa wilaya amesema kazi hiyo nzuri iliyoanzishwa na COSTECH kupitia Jukwaa la Bioteknolojia nchini (OFAB) hazitakuwa na maana endapo mafunzo hayo hayatasimamiwana halmashauri yake ili kuhakikisha yanakwenda kuleta mabadiliko na mapinduzi kwenye kilimo kwa wakulima kwenye maeneo mbalimbali. 

Kapufi amemtaka mkurugenzi wa halmashauri kuhakikisha anaweka bajeti kugharamia mafunzo ya aina hiyo kwa maofisa ugani na wakulima badala ya kuwaachia COSTECH kufanya kazi hiyo peke yao wakati wanufaika ni wananchi wa wilaya hiyo na hivyo kuahidi kuzungumza na wawekezaji wenye migodi kuweka bajeti kusaidia kilimo kwenye fedha mbalimbali zinazotolewa nao kwaajili ya maendeleo ya halmahauri.

Amesema anatambua kuna wakulima wengine hawapendi kubadilika pale wanapofikishiwa utaalamu lakini amewataka maofisa ugani hao kuto kata tamaa na badala yake wawe na mashamba yao binafsi ya mfano ambayo yatalimwa kwa kutumia kilimo cha kisasa na mbegu bora ili waone badala ya kuzungumza kwa nadharia kila siku.
Mratibu wa Jukwaa la bioteknolojia kwa maendeleo ya kilimo nchini OFAB bwana Philbert Nyinondiakizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo.


Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya hiyo Ali Rajabu, amewapongeza watafiti hao kutoka COSTECH,OFAB na Kituo cha utafiti wa Kilimo Ukiriguru cha Mwanza kwa kusaidia kuwawezesha maofisa ugani hao kupata mbinu bora zaidia za kukabiliana na changamoto za kilimo kwa wakulima kwa kutumia teknolojia za kisasa na kuiomba Halmashauri kuwapa vitendea kazi maofisa ugani wanaofanya vizuri kwenye kata zao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...