Kwa niaba ya Manispaa ya Kigoma Ujiji naomba kuchukua fursa hii kuushukuru Ubalozi wa China nchini, Balozi pamoja na Timu ya Wawekezaji kutoka China waliokuwa wageni wetu hapa Ujiji kwa muda wa siku 3. 

Ujio wao ni jambo lenye faraja kwetu kwamba juhudi zetu za kuainisha fursa za uwekezaji hapa  Kigoma (kupitia mwongozo wa Uwekezaji Kigoma Ujiji - Kigoma Ujiji Investor's Guide) zimeanza kuzaa matunda na kuvutia uwekezaji kutoka maeneo mbalimbali duniani.
Ziara ya Balozi Lu Youqing na timu yake imewezesha makubaliano kwenye maeneo matano (5) ya uwekezaji:
1. Ujenzi wa Kiwanda cha kuchakata Samaki na mazao ya Samaki katika mji wa Katonga, Kata ya Bangwe.

2. Ujenzi wa Kituo cha Biashara Ujiji (Ujiji City - The Great Lakes Trade and Logistics Center) katika kata ya Kitongoni na Kasimbu.
3. Uwekezaji Wa Kiwanda cha kusindika mazao ya michikichi.
4. Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Vijana eneo la Mwanga Community Center.
5. Ukarabati wa Soko la Ujiji na jengo la watumwa na ujenzi wa barabara ya watumwa ili kukuza Utalii na Ujenzi Mwalo wa Katonga.

Ziara ilikuwa ya mafanikio makubwa sana, ikitufikisha hata katika maeneo ambayo ni nadra mabalozi kufika (kama pichani tukivuka mto Luiche), ninaamini kuwa wananchi wa Kigoma watafanikiwa na miradi hii inayotokana na mahusiano mazuri kati ya nchi yetu na Jamhuri ya watu wa China. 
Ni dhamira yetu kuhakikisha tunautumia muda wa dhamana yetu tuliyopewa na wananchi kushirikiana nao kuleta maendeleo na kuipeleka mbele Kigoma Ujiji.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Mbunge, Kigoma Mjini - ACT Wazalendo 
Kigoma 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...