Na Dotto Mwaibale, Lindi

MAOFISA ugani mkoani Lindi wamesema wanashindwa kuwahudumia kikamilifu wakulima kutokana na kukosekana kwa usafiri wa kuwapeleka vijijini pamoja na kutelekezwa na wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi kwa kushindwa kuwapatia mafunzo ya mara kwa mara.

Wakizungumza juzi katika mafunzo kuhusu kilimo bora yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia, COSTECH, maofisa ugavi hao walisema kutokana na upungufu wa wataalam hao wamekuwa wanahudumia vijiji vingi na mtu mmoja anaweza kuhudumia vijiji hadi sita. 

Pia walisema kwamba tatizo lignine wamekuwa hawapati mafunzo ambayo yatawezesha waweze kwenda na wakati.

Ofisa Ugani kutoka Manispaa ya Lindi Hussein Mwapili alisema wizara ya kilimo baada ya kuwakabidhi maafisa ugani kwa halmashauri imeshindwa hata kuwafuatilia na hata kuwajengea nyumba wakati wizara zingine kama elimu na afya zinawakumbuka wataalamu wao kwa kuwajenge nyumba na kuwapa miongozo ya mara kwa mara.

“Sisi tumesahulika kabisa, tunakumbukwa wakati wa njaa tu ndipo utaona tunalaumiwa kwamba tunaishi mjini, lakini wizara ya kilimo imefanya nini kuhakikisha maafisa ugani wanaishi katika mazingira bora ya kufanyia kazi? Kule vijiji tunaambiwa tukaishi huko je kuna nyumba za wagani? alihoji.
Mwezeshaji kutoka Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Dk.Emmarold Mneney (kulia), akitoa mafunzo ya siku moja ya kilimo chenye tija kwa maofisa Ugani wa Mkoa wa Lindi kwenye Maonyesho ya Kitaifa ya Nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya Ngongo mkoani hapa juzi.
Ofisa Kilimo kutoka Manispaa ya Lindi, Amina Pemba akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Maofisa Ugani wakipata mafunzo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...