Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Christine Mndeme leo amezindua mradi wa Maji katika kijiji cha Mhande,Kata ya Ngh’ong’hona ambao umefadhiliwa na Shirika shirika la wamishionari wa damu takatifu ya Yesu(CPPS) uliogharimu kiasi cha Sh.Milioni 35.

Mradi huu umetokana na maombi ya Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde kwa Shirika la hilo kusaidia kutatua changamoto ya Maji katika kata hii ya Ngh’ongh’ona ambayo wananchi wake wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo kubwa la upatikanaji maji safi na salama.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mndeme amelishukuru shirika hilo la CPPS kwa ufadhili wa mradi huo na kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde kwa kuwa mstari wa mbele kutatua kero za wanachi wake hususani kero kubwa ya Maji katika kata ya Ngh’ongh’ona.

Amesema kutatuliwa kwa kero hiyo kumewatua kina mama ndoo kichwani kwa kuwa walikuwa wakienda kuchota maji umbali mrefu.

“Mwili unahitaji maji unapotafuta maji mbali roho inasononeka hata muda wa kusali unaukosa, tunashukuru sana shirika hili lakini wananchi tuna wajibu wa kuutunza mradi huu ambao ni wa thamani kubwa sana,”amesema

Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine Mndeme akifurahi jambo na wafadhili wa mradi wa maji wa Mhande kutoka Canada. 
Wananchi wa Mhande wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Chritine Mndeme katika uzinduzi wa mradi wa maji wa kijiji hicho. 
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine Mndeme pamoja na Father Fransis wakifungua bomba la maji kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji katika  kijiji cha Mhande. 
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christine Mndeme akisalimiana na father Fransis .


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...