THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Dkt. Chamuriho, MAB wakagua ujenzi Kiwanja cha ndege cha Songwe

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Serkta ya Uchukuzi), Dr. Leonard Chamuriho leo kwa kushirikiana na Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (MAB), wamefanya ukaguzi wa miundombinu ya barabara ya kutua na kuruka kwa ndege na jengo la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Songwe Mbeya.

Tayari ujenzi wa barabara ya kutua kwa ndege yenye urefu wa km. 3.3 umekamilika ambapo inaruhusu kutua kwa ndege zenye uwezo wa kubeba abiria kuanzia 90 hadi 300, ambapo ndege za mashirika mbalimbali ikiwemo ya ATCL, Precisions na Fastjet zimekuwa zikifanya safari zake mara kwa mara kwenye kiwanja hiho.
Kiwanja hicho kipi daraja la sita (category 6), ambapo mbali na ndege za abiria pia kinaruhusu kutua kwa ndege za mizigo ya mazao ya kilimo yakiwemo maua, matunda, nyama, mchele na maharage kupelekwa maeneo mbalimbali nchini na nje ya nchi.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Dr. Leonard Chamuriho (wa pili kutoka kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (MAB), Prof. Ninatubu Lema (wa pili kutoka kushoto), Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Salim Msangi (wa kwanza kushoto) na wajumbe wengine wa MAB wakisikiliza maelezo yanayohusu jengo la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa Songwe kutoka kwa wahandisi, walipotembelea ujenzi huo leo.
 Katibu Mkuu wa Wizara Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Drk Leonard Chamuriho (kulia) akitoka ghorofa ya kwanza ya jengo la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Songwe, Mbeya, mara baada ya kufanya ukaguzi na wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (MAB). Wanne ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Salim Msangi.
 Katibu Mkuu wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya Uchukuzi), Dr. Leonard Chamuriho (aliyechuchuma) akishika upana wa barabara ya kuruka na kutua ndege ya Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Songwe baada ya kupata maelezo kutoka kwa Wahandisi Washauri wa Kampuni ya UNETEC. Mhandisi Roupina Jambazian na Geofrey Asumenye (walioinama), baada ya kufanya ziara pamoja na wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Viwanja vya ndege (MAB) ya kukagua maendeleo ya ujenzi  wa miundombinu.
Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (MAB) na Katibu Mkuu wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya Uchukuzi), Dr. Leonard Chamuriho (wa kwanza kushoto)  wakikagua barabara ya kutua na kuruka kwa ndege ya Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Songwe. Wa pili kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vyua Ndege Tanzania (TAA), Bw. Salim Msangi.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA