THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

HALMASHAURI YA MERU YAONGOZA KWA USAFI WA MAZINGIRA KATI YA HALMASHAURI 185 ZA TANZANIA.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto, akizungumza na waandishi wakati akitangaza matokeo ya mashindano ya afya na Usafi wa Mazingira leo jijini leo jijini Dar es Salaam.kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Mohamed Kambi.

 Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii.
HALMASHAURI ya Meru uliypo mkoani Arusha inaongoza kwa asilimia 96  kwa usafi wa ujenzi wa na matumizi ya vyoo bora katika kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira iliyohusisha halmashauri 185.

Hayo ameyasema leo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto, Ummy Mwalimu wakati akitangaza matokeo ya mashindano ya afya na Usafi wa Mazingira leo jijini, amesema kuwa halmashauri ya Meru imeweza kufanya vizuri usafi wa mazingira na matumizi ya vyoo bora pamoja na kuwa na sehemu ya kunawa mikono.

Amesema nafasi ya pili kwa  usafi wa mazingira na matumizi bora ya vyoo ni Halmashauri ya Njombe kwa asilimia 95.1 ikifuatiwa na Halmashauri ya Makete kwa asilimia 80.4.

Waziri Ummy amesema  katika kutekeleza kampeni hiyo  kwa upande wa kijiji bora na mtaa kwa usafi kwa vilivyoshindaniwa ni 80 , kijiji cha Kanikale kinaongoza  wilayanii Njombe kimeongoza asilimia 95.8 , nafasi ya pili imechukuliwa kijiji cha Nambala wilaya Meru kwa asilimia 95.3 na kijiji cha tatu ni Lyalalo kwa asilimia 93.5 wilayani Njombe.

Amesema majiji na Manispaa ambazo zimefanya kampeni  ya  usafi wa mazingira, vyoo bora pamoja na udhibiti wa taka ngumu kwa Manispaa ni Manispaa ya Moshi kwa asilimia 78.5 mshindi wa Pili Jiji la Arusha kwa 78.1 ikifuatiwa na Manispaa ya Iringa kwa asilimia 67.2 

Waziri Ummy amesema kampeni ya 2018 wataongeza ofisi za serikali, shule za msingi na sekondari kushindanisha katika usafi wa mazingira na vyoo bora.