Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF Mhe. Anne Makinda ametembelea Maonesho ya Nanenane katika Viwanja vya Nzuguni Mjini Dodoma ambapo alikuwa mgeni rasmi wa siku hiyo. Mhe. Makinda alisisitiza umuhimu wa kila mtanzania kuwa na bima ya afya ili kuwa na uhakika wa matibabu na kuweza kutimiza majukumu yake ya kila siku na kuepukana na umaskini.

Alisema ‘…. tunajua kuwa katika zama hizi tunatakiwa kuchapa kazi kama Mhe. Rais wetu anavyotuhimiza, lakini ili tuweze kuendana na kasi hii hatuna budi kuwa na uhakika na afya zetu na Serikali imetuletea utaratibu huu wa bima ya afya ambao ni rahisi kwa kila mtu kujiunga na kuwa na uhakika wa matibabu pindi anapougua”

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Bernard Konga amesema NHIF imejipanga kutoka na kwenda kuwafuata watu walipo ili kuweza kuwasajili na huduma za Mfuko huo. Alisema kwa sasa Mfuko unafanya kampeni ya uhamasishaji wa huduma ya bima ya afya kwa watoto walio chini ya miaka 18 ijulikanayo kama TOTO AFYA KADI. “Mfuko umeanza kufanya usajili kwa wingi katika maeneo mbalimbali karibu na watu walipo ambapo kila mtoto anachangiwa sh. 50,400 tu kwa mwaka” alisema Bw. Konga.

Huduma hii ya TOTO AFYA KADI imezinduliwa rasmi na Waziri wa Afya Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wiki iliyopita ambaye alisema kuwa watoto ambao ni asilimia 51 ya watanzania wote wanahitaji kuwa na uhakika wa matibabu na alihimiza kuweka mikakati madhubuti kuhakikisha watoto hawa wanapata huduma hiyo.

Naye Meneja wa NHIF Mkoani Dodoma, Bi. Salome Manyama amesema wazazi na walezi wamepata mwitikio na kufika kusajili watoto wao katika huduma ya TOTO AFYA KADI katika maonesho hayo. Ameongeza kusema kuwa umma uko tayari na wamejipanga kuendeleza kampeni hiyo katika maeneo ya karibu zaidi na wananchi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF Mhe. Anne Makinda akisaini
kitabu cha wageni kwenye banda la NHIF jijini Dodoma alipotembelea maonesho ya Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya Nzuguni jijini humo.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Bernard Konga na viongozi wengine wa NHIF wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF alipotembelea banda hilo Jijini Dodoma kwenye maonesho ya Nanenane.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NHIF Mhe. Anne Makinda akisalimiana na mmoja wa maofisa wa NHIF waliokua wakishiriki maonesho ya Nanenane Jijini Dodoma.

Meneja wa NHIF mkoani Dodoma Bi. Salome Manyama akielezea jambo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NHIF Mhe. Anne Makinda ambaye
pia alitembelea banda hilo kama mgeni Rasmi wa maonesho hayo ya Nanenane yaliyokua yakifanyika jijini Dodoma kwenye viwanja vya Nzuguni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...