THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

NITASHIRIKIANA NA KLABU ZA MPIRA KWA MAENDELEO YA TFF- MADEGA

⁠⁠⁠Na Agness Francis, Globu ya Jamii 
Mgombea nafasi ya urais wa shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF),Iman Omary Madega amesema atashirikiana na klabu za soka kwa ajili ya kuleta maendeleo ya soka ya nchini pamoja na kuhakikisha wanapatikana wadhamini watakaosaidia maendeleo zaidi.
Madega ambaye ni mwanasheria wa kujitegemea, pia aliwahi kuwa mwenyekiti wa klabu ya Yanga amenadi sera zake leo Jijini Dar es salaam  kuelekea uchaguzi mkuu wa TFF unaotarajiwa kufanyika Agosti 12 Mkoani Dodoma.
 Akinadi Sera zake ambazo zinalenga hasa katika uadilifu,utendaji na uwazi amesema kuwa atakuwa bega kwa bega na klabu zote bila kubagua endapo atachaguliwa kuwa Rais wa shirikisho la kabumbu nchini kuachilia mbali kuwa aliwahi kuwa mwenyekiti wa klabu ya Yanga mwaka 2005-2010 chini ya uongozi wa Leodger Tenga na kuwataka wapenda soka kuondoa shaka kwa hilo.
Madega amesema ili kuweza kuongoza vizuri tasnia hii ya soka inaitaji muda ili kufanikisha utendaji mzuri wa kazi na kupiga hatua mbele zaidi katika soka.
 Mgombea huyo amesema lengo lake ataakikisha analeta mafanikio katikan sekta ya soka nchini kwa kuwapandisha Tanzania kutoka viwango vya sasa 120 vilivyopo kwa sasa na kushuka zaidi chini ili kuwa katika viwango bora duniani.
Katika soka la wanawake, Madega amehakikisha kuwa atatenga bajeti ya kutosha itokanayo na wadhamini ili waweze kucheza soka la mikoa yote nchini ili kukuza vipaji zaidi na ili kuwa na maendeleo hayo na kufikia hatua ya kimataifa atahakikisha anaboresha mahusiano mazuri kati ya TFf na serikali yetu,kuboresha viwanja vya mpira nchini, pamoja makocha wazuri na waamuzi wenye uwezo mkubwa wa kuchezesha mechi za kimataifa.


 Madega ametoa wito kwa wapiga kura kumchagua kuwa kinara katika uchaguzi huo wa shirikisho La soka Tanzania (TFF) utakaofanyika tarehe 12 agosti mwaka huu mjini Dodoma.
Mgombea nafasi ya urais wa shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF),Iman Omary Madega akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, wakati wa kunadi sera zake kati kampeni za kuwania nafasi hiyo, ambayo uchaguzi wake unatarajiwa kufanyika Agosti 15, 2017 mjini Dodoma.
 Mgombea nafasi ya urais wa shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF),Iman Omary Madega akiendelea kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo