Afisa Muuguzi Mwandamizi, Gudila Mambacho (kushoto) wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akichukua vipimo vya presha toka kwa mmoja wa wananchi (kulia) waliojitokeza kupata huduma za afya bure zinazotolewa na Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili chini ya udhamini mkuu wa Benki ya NMB jijini Dar es Salaam. Mmoja wa maofisa kutoka Benki ya NMB (kushoto) akimuhudumia mwananchi aliyejitokeza kupata huduma za kibenki kwenye kongamano la Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo mbali na huduma hizo za kibenki toka NMB, wananchi walipata huduma mbalimbali za afya bure, ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya siku ya wakunga duniani. Muuguzi mwandamizi na afisa lishe kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dotto Msabila Kafulie (kushoto) akimuhudumia mmoja wa wananchi aliyejitokeza kupata huduma za afya bure zinazotolewa na Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili chini ya udhamini mkuu wa Benki ya NMB jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...