Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) linashiriki maonyesho ya
Kilimo yanayoendelea mkoani Morogoro, Katika maonyesho hayo
wakazi wote wa Morogoro Hususan Wakulima wanakaribishwa
kupata elimu kuhusu namna ya kushiriki kilimo cha miwa
(Outgrowers Scheme) Mpango huu umeanziishwa mahususi ili
kuwasaidia watanzania kupata kipato kwa kulima miwa na Miwa
hiyo itanunuliwa moja kwa moja na Kampuni Hodhi ya Mkulazi
ambayo ni ubia kati ya NSSF na PPF.
Vile vile wananchi wote
wanakaribishwa kujiandikisha na NSSF ili kupata Matibabu bure
kwa mwanachama na wategemezi wake pamoja na Mafao
mengine yatolewayo na NSSF kama vile Mafao ya uzazi, kuumia
kazini, Mafao ya urithi, Pensheni ya uzeeni na mengineyo
Afisa wa NSSF Mr Shaban Salehe akimwandikisha mwanachama
mpya katika banda la NSSF katika maonyesho ya Nanenane
yanayoendelea mkoani Morogoro.
Afisa wa NSSF, Mwanawetu Njozi (kulia) akiongea na mgeni alietembelea banda la NSSF katika maonyesho ya Nanenane yanayoendelea mkoani Morogoro.
Afisa wa NSSF, Jonathan Mkahala akimwandikisha mwanachama mpya katika banda la NSSF katika maonyesho ya Nanenane yanayoendelea mkoani Morogoro, Pembeni kushoto ni Afisa mwandamizi wa Matekelezo wa Shirika hilo, Bw. Salawa.
Afisa Mwandamizi wa Masoko na Uhusiano, Amina Mbaga
akizungumza na wageni walietembelea banda la NSSF katika
maonyesho ya Nanenane yanayoendelea mkoani Morogoro.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...