Na Mwamvua Mwinyi, Pwani.
KAMANDA wa polisi mkoani Pwani,(ACP) Jonathan Shanna (Pichani Kulia), amesema kuanzia sasa watataifisha mali zote za watu wanaojihusisha na biashara ya usafirishaji wa wahamiaji haramu.

Aidha amewatahadhalisha wale wanaotoa vyombo vyao vya majini na nchi kavu kusafirisha wahamiaji hao  kwani navyo vitataifishwa .

Akizungumzia hatua walizozichukua kwa wahamiaji haramu 72 waliokamatwa mapema wiki hii,kamanda Shanna alisema kushiriki kwenye biashara hiyo ni kosa la kubwa la kijinai.

Amesema wanaojihusisha kusaidia na kuwawezesha kufika wahamiaji haramu watawachunguza mali mbalimbali walionazo kama imetokana na utakatishaji fedha na endapo itabainika imetokana na biashara hiyo zitafilisiwa.

Kamanda Shanna alibainisha,wataiomba mahakama kutaifisha mali zote za wale watakaobainika kuhusika kupata mali hizo na fedha na biashara haramu.

Amesema sheria ipo wazi inasema watu hao wapewe kifungo ama kupigwa faini hivyo itapendeza na itafurahisha jeshi la polisi kama watakuwa wanapewa adhabu zote na kufungwa .

Kamanda Shanna ,alisema taarifa ikifika makwao kuwa wanafungwa na kupewa adhabu kali ndipo wataacha kuingia nchini kwani watajua Tanzania sio mahala pa mchezo wala kukimbilia.

“Hii kuwakamata kuwapiga faini na kuwarudisha kwao ndio maana wanafanya mchezo mchezo kukimbilia huku,ukiwapiga faini wanakwenda wanarudi ni mchezo wa kuigiza”alisema .

Kamanda Shanna alielezea kwamba,Tanzania ina sheria zake endapo sheria zitawabana wahamiaji hao na kukoma kugeuza nchi kuwa lango lao la kupita kwenda nchi jirani ikiwemo Afrika ya kusini.

Hata hivyo ,kamanda huyo alisema wahamiaji waliokamatwa wameshawafikisha ofisi ya uhamiaji mkoani hapo na watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.


Jeshi hilo,linaendelea kudhibiti wahamiaji haramu ili kupungua wimbi kubwa linaloingia kupitia njia za panya mkoani hapo hasa bandari bubu 18 zilizopo Bagamoyo .

Pamoja na hilo,Kamanda Shanna alisema wanafanya oparesheni kusaka wahalifu mbalimbali ,zoezi ambalo ni endelevu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...