THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Bunge la Tanzania kuanzisha Urafiki wa Kibunge na Bunge la UAE

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai leo ametembelea Bunge la Umoja wa Falme za Kiarabu na kufanya mazungumzo na Spika mwenzake, Dr Amal Al Qubaisi ambapo amewasilisha mapendekezo rasmi ya kuanzisha Umoja na Urafiki wa Kibunge baina ya Bunge la Tanzania na Bunge la Umoja wa Falme za Kiarabu.

Mhe Spika Al Qubaisi ambae ni Spika wa kwanza mwanamke katika nchi zote za Mashariki ya Kati kwa niaba ya Bunge la nchi hiyo amekubali mapendekezo hayo na kutoa mwaliko Kwa Wabunge wa Tanzania kutembelea Bunge la Umoja wa Falme za Kiarabu kwa nia ya kuona namna  UAE ilivyopiga hatua.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Bunge la Umoja wa Falme za Kiarabu, Abu Dhabi. kulia kwake ni Spika wa Bunge hilo, Dr Amal Al Qubaisi. 
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai akiwa na mwenyeji wake, Dr Amal Al Qubaisi baada kuzungumza nae.
Spika Job Ndugai akipewa ziara ya Bunge la nchi hiyo na Spika Al Qubaisi