Tanzania imetajwa kuwa nchi ya kwanza Kusini mwa Afrika kuanza kutumia  mfumo wa kielektroniki wa PlanRep ulioboreshwa ambao husaidia katika mipango, bajeti na kutoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini kote.

Akizungumza katika mahojiano maalum mjini Kigoma, Mkuu wa Timu ya Mifumo ya TEHAMA kutoka mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)  Desderi Wengaa, amesema kuwa  mfumo huo utasaidia Taifa kufikia maendeleo endelevu kwa wakati kwani utaunganishwa na mifumo mingine iliyopo sasa na utawashirikisha wananchi wote.

“Mfumo huu utawezesha kutolewa kwa taarifa za miradi ya maendeleo zinazohusu sekta zote zilizoainishwa katika mipango na bajeti kwa wakati katika kipindi chote cha mwaka” alisema Wengaa.

Aliendelea kusema kuwa PlanRep iliyoboreshwa inaunganisha sekta zote katika mfumo mmoja ambao ni wa kitaifa tofauti na ilivyokuwa awali ambapo kila sekta ilikuwa na mfumo wake. Awali mfumo uliokuwa ukitumika haukuwa unaendana na mahitaji ya wakati hivyo kushindwa kufanya uchambuzi wa kina katika kusimamia rasilimali zilizokuwepo ikiwemo fedha. 

Aidha,watumiaji wa mfumo huo  wataweza kuutumia mahali popote  kwa kuwa ni wa kitaifa na utaondoa changamoto ya kuwepo kwa matoleo tofauti tofauti. Hali hii itasaidia kuokoa fedha nyingi zilizokuwa zikitumika kwa watoa huduma wa mifumo ya awali katika halmashauri na mikoa yote nchini.
Kiongozi wa Timu ya wataalamu wanaofanya maboresho ya mfumo wa kielektroniki wa PlanRep, Bi. Nseya Kipilyango akizungumza wakati wa mafunzo kwa watumiaji wa mfumo huo yanayoendelea Mjini Kigoma.
Mmoja wa Wawezeshaji wa Mfumo wa mfumo wa kielektroniki wa PlanRep Kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bi Jacqueline Manyanga akiwasilisha mada kwa watumiaji wa mfumo huo yanayofanyika Mkoani Kigoma yakihusisha Mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma.
Washiriki wa Mafunzo wakifuatilia mada wakati wa mafunzo hayo yanayoendelea mjini Kigoma.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...