By Bushiri Matenda-MAELEZO

Licha ya kuyumba kwa uchumi na kuongezeka kwa mfumuko wa bei duniani, Tanzania imeendelea kuongoza kwa ukuaji wa uchumi miongoni mwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo takwimu za Benki Kuu ya Tanzania (BOT) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) zimetaja uchumi wa Tanzania kuwa imara.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi alibainisha hayo wakati akitoa ufafanuzi kwa Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusu hali ya uchumi nchini.

“Uchumi wa Tanzania kwa miaka mitatu mfululizo sasa bado uko katika ukuaji usiopungua asilimia 7.0 hadi 7.2 ikiwa ni ukuaji wa juu katika ukanda wa Afrika Mashariki ambapo Rwanda inakua kwa asilimia 6, Uganda asilimia 5 na Kenya asilimia 6.4”, alisema Dkt. Abbasi.

Alieleza kuwa sambamba na ukuaji wa uchumi, Tanzania imeendelea kudhibiti mfumuko wa bei ambapo taarifa ya hivi karibuni zilizotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) zinaonesha kuwa mfumuko wa bei nchini umeshuka kutoka asilimia 6.1 mwezi Mei hadi kufikia asilimia 5.4 mwezi Juni mwaka huu.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya uchumi nchini leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara hiyo Sehemu ya Habari na Picha Bw. Rodney Thadeus.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Hassan Abbasi (hayupo pichani) alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu hali ya uchumi mbele ya waandishi wa habari leo Jijiji Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Hassan Abbasi akiwasilisha mada kuhusu hali ya uchumi wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.
Picha zote na: MAELEZO.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...