Ujerumani imeipatia Tanzania kiasi cha Euro milioni 198.5 sawa na Sh. Bilioni 520.86 zilizotumika kufadhili miradi mbalimbali ikiwemo ya Maliasili na Mazingira, Afya, Maji, Nishati, Udhibiti wa Fedha za Umma (Good Financial Governance) na Kusaidia Huduma za Wakimbizi katika mkoa wa Kigoma, katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban wakati wa tukio la Tanzania na Ujerumani kusaini kumbukumbu za Mkutano wa Mashauriano ya Kimaendeleo (Bilateral Development Consultations) ambapo Ujerumani imeonesha nia ya kuendelea kuisaidia Tanzania katika Sekta hizo kuanzia mwaka 2018 hadi 2021.

Kumbukumbu za Mashauriano hayo zimesainiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Naibu Mkuu wa Idara ya Kanda ya Afrika Mashariki katika Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Ujerumani Bw. Georg Rademacher kwa niaba ya Serikali ya Ujerumani. 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban (kushoto) na Naibu Mkuu wa Ushirikiano wa kiuchumi Kanda ya Afrika Mashariki kutoka Ujerumani Bw. Georg Rademacher wakibadilishana kumbukumbu za Mkutano wa Mashauriano baada ya kusainiwa katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Wajumbe kutoka Ujerumani waliohudhuria Mkutano wa Mashauriano ya Maendeleo kati ya Tanzania na nchi hiyo wakisikiliza kwa makini maelezo ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban (hayupo pichani) akieleza mafanikio ya msaada wa nchi hiyo katika Nyanja za Afya, Maji, Nishati na Utawala wa Fedha, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Maafisa waandamizi kutoka Tanzania wakifuatilia kwa makini Mkutano wa Mashauriano ya Kimaendeleo kati ya Tanzania na Ujerumani yaliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Dkt. Detlef Wachter (wa pili kushoto) akizungumza kuhusu nia ya nchi yake kuisaidia Tanzania katika miradi ya Nishati, Maji, Utawala wa Fedha na Afya kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo kuanzia mwaka 2018, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban (wa nne kushoto) na Naibu Mkuu wa Ushirikiano wa kiuchumi Kanda ya Afrika Mashariki kutoka Ujerumani Bw. Georg Rademacher (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa waandamizi kutoka Ujerumani na Tanzania baada ya kusainiwa kwa kumbukumbu za Mkutano wa Mashauriano, katika ofisi za  Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Mamelta Mutagwaba akipeana mkono na Naibu Mkuu wa Ushirikiano wa Kiuchumi Kanda ya Afrika Mashariki kutoka Ujerumani Bw. Georg Rademacher (kushoto) baada ya kusainiwa kumbukumbu za Mkutano wa Mashauriano ya Maendeleo kati ya nchi hizo mbili Jijini Dares Salaam.
Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Mamelta Mutagwaba akisalimiana na Wajumbe wa Mkutano wa Mashauriano ya Maendeleo kati ya Tanzania na Ujerumani, katika viunga vya Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango).



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...